Serikali ya Australia  itapeleka kundi la wataalamu nchini Dubai kwa ajili ya kujadili njia za kuendeleza uchumi unaofuata sheria za kiIslam nchini Australia. Ujumbe huo utakaongozwa na mtaalamu wa kiuchumi wa Australia ndugu Barry O’Farrell  na wataalamu wengine wa mambo ya kiuchumi, watajadili maswala mazima yanayohusiana na usimamizi na sheria za uchumi huo, wakati  huohuo ujumbe huo utatembelea mji wa Abu Dhabi na Lebanon.
Australia ina mategemeo ya kua na mchango mkubwa ktk uchumi huo kwa kuzingatia kwamba nchi za kusini mashariki mwa Asia ambazo zina uhusiano wa karibu na nchi hiyo, uchumi unaofuata sheria za kiIslam unakua kwa kasi. Moja ktk matatizo yaliyopo ni pamoja na uhakika kwamba juhudi za kupitisha sheria ya kuuruhusu uchumi huo kasi yake ni ndogo sana ktk ngazi za juu, kitu ambacho kimeilazimisha serikali ya Australia  kuingilia kati. Serikali ya Austaralia ina hamu kubwa ya kujihusisha na uchumi huo alisema Salim Farrar muhadhiri mkuu  wa kitengo cha sheria  ktk chuo kikuu  cha Sydney ambae alikiri vilevile kwamba swala hilo linahitaji mtiririko wa majadiliano ya kisiasa.
Pamoja na mambo mengine Australia inakabiliana na changamoto zinazohusiana na sheria mpya za uchumi unaofuata sheria za kiislam hususan ktk maswala mazima ya Islamic bonds na triple tax duties. Kwa maelezo zaidi wasiliana na http://ijuebankyakiislam.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ni habari njema kwa waislam na wsiokua waislam. Matatizo ya uchumi yanayoukumba ulimwengu yamesababishwa na vitu vingi ikiwemo riba, kutokua na uwazi uwazi ktk biashara nyingi, makisio ya faida yenye hatari kubwa yasiyolindwa na rasilimali na mengineyo kama vile kukataa kugawana hasara na faida ktk biashara na badala yake upande mmoja tu kubeba majukumu hayo peke yake. Ni wakati muafaka wa kuangalia njia mbadala za uchumi ambao unachunga sana maadili kuliko kuangalia faida tu.

    ReplyDelete
  2. mtume muhammad hakika amesema ukweli na tunashuhudia.

    Sasa wamejua umuhimu wakufuata mfumo wakibiashara wakiislaam. Tatizo lakiichumi linaloikabili dunia pure inatokana na riba.

    ReplyDelete
  3. Uchumi wa Kiislamu,

    Pana watu wana dhana potofu juu wa Uislamu na kupelekea kujenga chuki zisizo na msingi dhidi ya Uislamu kitu ambacho hakisaidii.

    Kama kanunu za Kisayansi zimethibitisha Mfumo wa Kibenki na Uchumi wa Kiislamu ni suluhisho, je kwa nini binaadamu anapinga?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...