Kama ulishawahi kufika au kakaa Zanzibar,basi ni lazima utakuwa unapajua kama si kuwa umefika sehemu hii ya Bustani za Forodhani (wenyewe hupenda kupaita Foro) iliopo maeneo ya Mji Mkongwe kisiwani hapa.kwani kila siku inapofika wakati wa jioni,eneo hili ndio linashamiri kwa biashara mbali mbali za vyakula vya kila aina na hukusanya watu wengi kutoka sehemu mbali mbali na ndani na nje ya Zanzibar.Kamera ya Globu ya Jamii leo imefanikiwa kuzinasa taswira kadhaa za namna hali inavyokuwa katika eneo hili na baadhi ya vitu vinavyopatikana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Hii ndo raha ya kisiwa cha marashi ya karafuu, dah.... naona Mr. Issa hapa unatutamanisha na mambo ya Seafood tu hapa...

    ReplyDelete

  2. Chunga sana mishkaki ya maini hapo,Kokoni nyumba nzima tuliwahi kuendesha!

    ReplyDelete
  3. wee michuzi unanitamanisha kama nini vipocho pocho vya nyumbani bwana next time please usiviweke mwenzio nahuzuni huku majuu niko kama mfungwa siwezi kwenda kwetu halafu unaweka vipocho pocho vya nyumbani umenifanya nimelia sana tena sana kwa ku miss home sick.

    mdau NY

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sasa we huko NY unang'ang'ania nini na huo upweke wako?!

      Delete
  4. hapa nimekubali.Hata huko Ulaya na America hakuna utamu kama huu, halafu vyakula vyote ni fresh, Kweli Bongo ni tambarare na Zanzibar.Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  5. Bahati mbaya siku hizi forodhani imevamiwa na madalali mateja ambao ufanya usumbufu wa kupiga debe kushawishi wateja waende kununua meza fulani harafu wanapata chochote nadhani toka kwa wauzaji.Kitu ambacho hawajashtukia hawa wauzaji ni kwamba mateja hawa wanabughudhi watu na kuharibu hadhi ya forodhani,teja ni teja siku hizi wanaibia watalii pale pale. Kuna wauzaji wachache wenye msimamo wa kutoletewa watalii na mateja lakini nilipokwenda pale mapema mwaka huu mambo yalikua mabaya yaani wana harrass watalii. wahusika pale wawa swala hili kabla mambo hayajaharibika.

    ReplyDelete
  6. Hivi nani anaunza kisanvu huku ulaya - email address please!!

    ReplyDelete
  7. Asante sana Issa michuzi kwa kuniwekea home ground love zenji.

    ReplyDelete
  8. Aaaah! jamani wenyewe twapaita Foro! Hapakinai hata! There is no Zenj bila Foroshani jamani

    ReplyDelete
  9. USHAURI WA BURE:
    1) Ukiwahi sana kufika foro (let's say saa 12) utakula mishikaki ya jana iliyolala.

    2) Kama utaweza epuka sea food. mara nyingi vyakula kama kaa, pweza n.k havinunuliwi sana hivyo utakuta vimekaa siku nyingi (sometimes mpaka wiki)

    3) Juisi ya miwa, maji hayachemshwi. miwa yenyewe huparwa huko shamba na huletwa foro kwa mikokoteni bila kufunikwa

    4) Ushauri: fika kuanzia saa mbili usiku, kula chipsi, chapati, mishikakii(ng'ombe).

    5) kama huwezi masharti haya andaa FLAGYL kabisa

    ReplyDelete
  10. Huyo alieharisha hata ainywa maji anaharisha. Chakula hapo hot and fresh, organic.

    ReplyDelete
  11. Vyakula hapo wanasubiri Wazungu wanunue maana ni ghali sana. Tunaita vyakula VIMEDODA. Kipande kidogo tu cha pweza ni sh5000. Wakati sokoni pweza mzima ni sh5000. Mimi mwenyeji lakini maji ya miwa nayaogopa, lakini bora kuliko juice ya bongo maana maji ya Bongo ambayo ni machungu.

    ReplyDelete

  12. Yaani hapo unapiga mishikakii weeee halafu unachukua flight break ya kwanza Northampton, Serengeti Bar halafu unashushia fosters

    ReplyDelete
  13. Mbona hakuna umeme!??? kama sehemu inaingiza mapato ya taifa jamani hata kuweka umeme tunashindwa??? Siwezi kula sehemu kama hii, labda kwa vyakula vya moto vinavyotoka jikoni kama wadau walivyosema hapo juu. Inaonekana usafi sio kitu cha kawaida kama wadau kadhaa walivyosema hapo juu.

    ReplyDelete
  14. shukran mdau kwa kutuwekea masharti ya kwenda kula vinono time gani lakin pweza na sea food nazipenda sana mimi na juice ya miwa,sijui nitaanyaje nijianda kwa flagyl

    ReplyDelete
  15. kuna mtu hapa kamwambia mwenzake anafanya nini NY Wewe unafananisha NY NA BONGO Wewe acha hizo watu wakotayari kufa huku huku, mpaka wapate makaratasi kieleweke waje home ndo maisha ya huku wewe tunakufa na tai shingoni akija bongo utamsadia au domo kaya

    ReplyDelete
  16. unaetaka kisamvu nenda maduka ya wa west africa au wa Asia.Utapata zinauzwa kwenye packet imeshakatwa katwa badhani wanatayarisha viwandani na kuwa frozen.
    taste yake kama kawa karibia na ukiwa hm

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...