Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tanga Mhe. Amina Mwidau (CUF), akipata maelezo kutoka kwa  mzalishaji wa vipindi Catherine Sekibaha, kulia ni Meneja wa Pangani FM Ismail Mwishashi pamoja na Mhariri wa Habari wa Radia hiyo Richard Katuma.
 Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tanga Mhe. Amina Mwidau (CUF), akipata maelezo  kutoka kwa Mhariri wa Habari wa Pangani FM  Richard Katuma, katikati ni mtangazaji wa zamu Bakari Kiwingu, akiwajibika.
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tanga Mhe. Amina Mwidau (CUF), akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa kituo cha Radia cha Pangani FM Ismail Mwishashi, kushoto pamoja na Mhariri wa Habari wa redio hiyo Richard Katuma aliyesimama kulia.


Na Mwandishi wetu, Pangani
MBUNGE wa Viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau, amesema ili jamii iweze kuendelea ni lazima ipate haki ya kupata habari za maendeleo yao.
Kauli hiyo aliitoa leo mjini hapa alipokuwa akizungumza na Meneja wa kituo cha Radia cha Pangani FM Ismail Mwishashi, alipokuwa akitimisha ziara yake wilayani Pangani kwa kutembelea kituo hicho.
Alisema kuwepo kwa Pangani FM, kumeweza kuisaidia jamii kupata elimu ya afya ya mama na mtoto pamoja na mapambano ya Ukimwi kwa kushiriki moja kwa moja kupiga simu kupitia vipindi vya redia.
“Pangani sasa itapaa kimaendeleo na jinsi Pangani FM inavyosafiri kwa mawimbi yake hasa kwa wakazi wa wilaya hii ya Pangani ni chachu kubwa ya maenendeleo. Sasa name kama mbunge nitakikisha ninapigia debe sekta ya utalii wa ndani hasa kwa kuvitangaza vivutio vya wilaya yetu,” alisema Mwidau
Kwa upande wake Meneja wa Pangani FM Ismail Mwishashi, alisema  redio yao imefanikiwa kupata kundi kubwa la wasilikizaji ambao hujifunza masuala mbalimbali yanayotangazwa kupitia radio yao.
“Pangani FM tunatangaza taarifa za habari na tuna waandishi wetu ambao wameenea katika kila kata ya Wilayah ii ya Pangani na kupitia mfumo wetu huu tumefanikiwa kuwa na idadi kubwa ya wasikilizaji tangu kuanzishwa kwake Agosti mwaka jana,” alisema Mwishashi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...