Mchungaji Dr. Emmanuel Kandusi (kulia) , manusura, mwathilika wa saratani ya tezi dume (prostate cancer)  na mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus campaign yuko Washington DC kwenye Kongamano (Summit) la saratani ya tezi dume linaofanyika katika jengo la Maseneta wa Marekani Russell Hall Capitol Hill. 

Katika kongamano hilo ambalo limehudhuriwa na waathilika na wanaharakati wa saratani ya tezi dume na baadhi ya Maseneta na Wabunge (Members of Congress) unajadiri pamoja na mambo mengi umuhimu wa kutoa elimu katika jamii juu ya saratani ya tezi dume na umuhimu wa kutoa tiba ya kisasa kwa watu wote na mahali popote. 

Kongamano linalohudhuriwa na washiriki takribani mia moja, umeandaliwa na shirika la hiari Prostate Health Education Network la Marekani na lenye makao makuu huko Boston. Shirika hilo linakazia “Knowledge is the best defense against prostate cancer”. 

Kongamano liligundua kuwa kwa kutoa elimu katika jamii utawezesha kupunguza magonjwa ya saratani (prevention is better than cure) kwa watu wengi. Watu wakielimika na kupata elimu juu ya hali hatarishi, uuhimu wa kubadili maisha yao kwa kula vyakula asilia, kufanya mazoezi, kujiepusha na utumiaji wa tumbaku wa aina yote, kupiga vita unene hatarishi itapunguza sana watu kupata saratani. 

Hii itaokoa nguvu kazi na kuokoa pesa nyingi ambazo zinaweza kutumia kwa maendeleo mengine. Katika picha ni Dr. Kandusi akimkabidhi magazeti ya MAN Rais na Mwanzilishi wa Prostate Health Education Network Ndugu Thomas Ferington. Ndugu Farrington naye ni manusura, mwathilika na mhanga wa saratani ya tezi dume.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jamani hapa tuna "hero" ambaye ingefaa taifa limtambue. Kwa nini naye asipewe tuzo! Ahsante kutupatia elimu saratani ya tezi dume na pia kutuwakilisha hata uendapo huko ughaibuni. Mungu akubariki!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...