Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein  amemteuwa Abdulsalam Issa Khatibu kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Kilimo, Kizimbani.

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka  kwa Mkurugenzi wa Idara ya  Mawasiliano Ikulu, Bw.  Hassan Khatib, imeeleza kuwa Abdulsalam  anachukuwa nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo Makame Salum ambaye muda wake wa Kikazi ulimalizika.

Abdulsalam  Issa Khatibu aliwahi kuwa Mbunge wa CCM  wa Jimbo la Makunduchi na ni Mtaalamu wa mambo ya Kilimo ambaye alifanya kazi ndani na nje ya nchi katika Mashirika ya kimataifa.

Aidha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein amemteuwa Mayasa Salim Ali kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Mbadala Zanzibar.

Uteuzi huo umeanza tarehe 27Septemba 2012.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...