Mwenyekiti wa Salasala Vision Group (SVG) chja Salasala, Dar es salaam, Yahaya Mbanka akiongea katika hafla ya kukabidhi gari la polisi la doria ambalo kikundi hicho kilichanga zaidi ya shilingi milioni 2 kwa ajili ya matengenezo
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kawe, Gilles Muroto akizungumza katika hafla hiyo.
Waendesha bodaboda wa kituo cha Mbuyuni Kunduchi nje kidogo ya jijini Dar es Salaam wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vizibao 100 vilivyotolewa na SVG kwa ajili ya kuwatambua wakati wakiwa katika maeneo yao ya kazi hususani katika eneo la Salasala
Baadhi ya Askari wa doria waliohudhuriua hafla ya makabidhiano ya gari la Polisi
Inspekta a Modesta Msome akitoa maelekezo kwa waendesha bodaboda wa kituo cha Mbuyuni ili kujua umuhimu wa kufuata sheria za usalama barabarani wakati wa hafla ya kutoa vizibao 100 kwa waendesha pikipiki wa eneo la Salasala, mwishoni mwa wiki
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kawe, Gilles Muroto akimvisha mwendesha bodaboda, Patson Agustino moja kati ya vizibao maalum 100 vilivyotolewa na kikundi cha Salasala Vision Group kwa ajili ya kuwatambua waendesha pikipiki wa eneo hilo.
Gari la Polisi lililofanyiwa matengenezo na SVG
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kawe, Gilles Muroto akipokea gari la doria la Polisi lenye namba za usajili T332 ANV kutoka kwa Mwenyekiti wa Salasala Vision Group (SVG), Yahaya Mbanka baada ya kikundi hicho kujitolea zaidi ya sh. milioni 2 kwa ajili ya kulifanyia matengenezo gari hilo
SVG ni mfano wa kuigwa, keep it up guys. hiyo ni changamoto kwa umma kuwa si kula kitu tutegemee serikali. wanachi pia tunatoe michango yetu kwa maendeleo ya jamii. Mbona makanisani na misikiti tunatoa michango mingi ambayo hata mingine hatujui matumizi yake? Wa TZ wenzangu tuisaidie serikali yetu kwa manufaa yetu na vizazi vijavyo.
ReplyDeleterushwa za wazi hizo.
ReplyDeletetunazibariki kwa kuzipigia makofi.
Eneo la salasala lilijulikana kama kandahal kwa sababu za uhalifu wa kupiliza sasa tunapumua kidogo..kumbuka tukio km la kuuwawa kwa Prof.Mwaikusa,Mtui na Gwamaka na mengine mengi yamerudisha nyuma maedeleo ya familia na taifa kwa ujumla.Leo hii tumejichangisha na kulitengeneza gari ambalo lilikua bovu ili kusaidia patrol za maeneo yetu bado kuna pumbavy anasema tumetoa rushwa.Wewe unaesema hivyo si ajabu mtaaa unaokaa vibaka ni wengi na hujachukua hatua yoyote ya kukabili tatizo.Heshimu michango a wengine kwa ajili ya jamii nzima tafadhali.
ReplyDelete