Wanamuziki wakongwe wa bendi ya Muziki wa Dansi hapa nchini ya Msondo Ngoma (Baba ya Muziki) wakikamua vilivyo katika Ufunguzi wa Tamasha la wazi la Muziki wa Dansi Tanzania linaloendelea kufanyika usiku huu katika viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.Tamasha hili ambalo ni la kipekee katika tasnia hii ya Muziki wa Dansi,litafanyika kwa siku mbili mfululizo ikiwa leo ndio siku yake ya kwanza.
Wapulizaji wa Midomo ya Bata (Trampet na Sexaphone) wa Bendi ya Msondo Ngoma wakiongozwa na Roman Mng'ande a.k.a Romario (kulia) wakifanya vitu vyao katika Tamasha hilo usiku huu.
MCD akiendelea na libeneke lake la Kusakata Tumba ndani ya Mashujaa Band kwenye Tamasha la Wazi la Muziki wa Dansi hapa nchini linaloendelea kufanyika hivi sasa katika viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.
Kundi zima la Bendi ya Muziki ya Mashujaa wakiongozwa na Charles Baba (pili kushoto) wakikamua vilivyo kwenye Tamasha la wazi la Muziki wa Dansi hapa nchini linaloendelea hivi sasa katika viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam usiku huu.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...