1.  KUTOKANA NA MHESHIMIWA WAZIRI NA NAIBU WAKE KUWA NJE YA OFISI, KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AMEPOKEA RISALA YA WAISLAMU NA KWAMBA ATAIFIKISHA KWA WAZIRI MARA TU ATAKAPORUDI NCHINI.

2.  KATIKA MAZUNGUMZO KUNA MANENO KUWA KUNA WAISLAMU WAMEWEKWA NDANI KUTOKANA NA ZOEZI LINALOENDELEA LA SENSA.  KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, AMETOA AMRI KWA RPC WOTE KUSITISHA UKAMATAJI WA WATU KUTOKANA NA ZOEZI LA SENSA NA KWAMBA WATUHUMIWA WALIOKAMATWA WAACHIWE KWA DHAMANA.

3.  MAMBO MENGINE YOTE YALIYOTAJWA KWENYE RISALA YA WAISLAMU YATASHUGHULIKIWA MARA BAADA YA WAHESHIMIWA MAWAZIRI WENYE DHAMANA HIYO KURUDI NA MTAJULISHWA.

TAMKO LIMETOLEWA NA,

                                   Signed
MBARAK M. ABDULWAKIL
KATIBU MKUU
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
07 Septemba, 2012

Usuli: Leo tarehe 07 majira ya alasiri, baadhi ya waumini wa madhehebu ya Kiislamu waliandamana hadi Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiwa na hoja mbalimbali ambazo waliziandika kama Risala kwa lengo la kuziwasilisha kwa Waziri wa Mambo  ya Ndani ya Nchi.  Hata hivyo Waziri na Naibu wake wako safarini hivyo Risala hiyo ilipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara, Mbarak Abdulwakil, ambaye baada ya majadiliano alitoa tamko hili hapa juu kwa niaba ya Waziri.

(Imesambazwa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kukamata watu hakutasaidia chochote, set them free.
    Tunakoelekea si kuzuri ee Mola inusuru tanzania. All i know sisi ni masikini sana tusiige kinachofanyika nchi nyingine. We will never know kidogo tulichonacho ni muhimu sana mpaka tupoteze tukipoteze na tukikipoteza majuto yake ni makubwa na kukipata tena ni almost impossible kuna nchi nyingi sana wish to have what we have sisi tunachezea tulichonacho. haya maandamano mema na kudai kwema hizo haki.

    ReplyDelete
  2. Waziri akisafiri si Naibu anakaimu???
    Hii imekaaje

    ReplyDelete
  3. safi sana mdau hapo juu umesema kitu cha maana kabisa

    waachieni hao raia wa kitanzania wana haki ya kuchagua walitakalo kwenye nchi yao

    serikali acheni kutesa raia wenu pasipo na sababu maonevu mpaka lini?

    na huyo mheshimiwa waziri inakuaje anasafiri na naibu wake? ina maana ofisi imefungwa mpaka watakaporudi kutoka safari?

    chonde chonde viongozi wetu mnapotupeleka pabaya sana tanzania inawaka ndani pindi siku huo moto utakapotoka nje nafikiri hatopatikana wa kuuzima

    mungu ibariki tanzania.

    ReplyDelete
  4. Kama wamevunja sheria kwanini wasikamatwe?? Wizara ilitoa onyo kuwa ni kosa la jinai ikimkuta mtu hataki kuhesabiwa. Sasa inakuwaje waliokamatwa waachiwe? Je wengine waliokamatwa ambao sio waislamu nao itakuwaje?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...