Na Mwandishi Maalum, New York
Mkurugenzi wa Kitengo cha Polisi katika Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani ya Umoja wa Mataifa ( DPKO) Kamishna Ann-Marie Orler, ameiopongeza Tanzania kwa kuwa miongoni mwa nchi ambazo zimeitikia vema wito wa kuchangia kwa idadi kubwa askari polisi wanawake. Askari Polisi wanawake wanahitaji sana katika Operesheni za Ulinzi wa Amani kutoka na umuhimu wao katika kushughulikia masuala muhimu yanayohusu wanawake na watoto wa kike .
Umuhimu wao umemlazimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kujiwekea lengo la kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2014 idadi ya askari wanawake katika operesheni za kulinda amani inafikia asilimia 20 ya askari polisi wote. Kwa sababu hiyo Kitengo cha Polisi cha Umoja wa Mataifa, kimezitaka nchi zote ambazo zinaombwa kuchangia askari polisi zihakikishe kwamba kuna kuwa na uwiano sawa kati ya wanaume na wanawake na kwamba watatoa kipaumbele kwa wanawake katika uteuzi wao kwa kuzingatia pia uwezo na sifa zilizoainishwa na Umoja wa Mataifa na si kwa sababu tu ni mwanamke polisi.
Askari wa pili kushoto mstari wa kwanza amechapia
ReplyDeleteMaafande wa Kike si mchezo !
ReplyDeleteUsije ukaomba kukamatwa na Askari wa kike, lohhh mbona utakoma?
Ilikuwa Jumamosi ilikuja basi Doble coaster ya kuzuka haina ruti pale Stesheni Ijumaa ya tarehe 28 Septemba, 2012 tunelekea Mbagala saa 2.30 usiku, ile tunaingia ndani dereva anatoka Kituoni Trafiki wa kike alituona akakodi Teksi akatufukuza akatupata Mivinjeni akaamuru twende moja kwa moja hadi Kilwa Road Kituo cha Polisi, ilibidi tutafute usafiri mwingine Dereva na Konda tuliwaancha LUPANGO!!!
Haya wakina mama wapika Gongo Kigogo Mbuyuni Maafande wa Kike hao wanakuja wakiwa na bunduki mikononi na Gwaride lao !...mwageni ndoo za Gongo lenu mkimbie Msituni mutafungwaaa!!!
ReplyDelete