Treni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA),likiwa katika stesheni ya Dar es Salaam kabla ya kuanza safari ya Majaribio iliyofanyika kutoka Dar es Salaam-Mwakanga-Kurasini-Dar jna mchana. Treni hiyo kwa kuelekea Mwakanga itapita  Kwa fundi Umeme, Kwa Limboa, Lumo(Kigilagila), Sigara, Kitunda, Kupunguni B, Majohe, Magnus na Mwakanga. Na kuelekea Kurasini Itatokea Dar,Kwa fundi Umeme,Yombo,Chimwaga,Maputo,Mtoni Relini,Kwa Azizi Relini na kishia Stesheni ya Kurasini.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA)na wa Wizara ya Uchukuzi wakiwa ndani ya Mojawapo ya mabehewa yaliyofanyiwa majaribio kwa ajili ya Usafiri wa treni Jijini Dar es Salaam jana.

 Meneja Mkuu wa Kanda ya Tanzania wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA),Mhandisi Abdalla Shekimweri akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo jana wakati wa majaribio ya Mabehewa matatu yakayofanya safari zake kutokea Dar-Kurasini-Mwakanga.Mabehewa hayo ni sehemu tu ya mabehewa yatakayokuwa yakifanya safari hizo.

Meneja Mkuu wa Kanda ya Tanzania wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), Mhandisi Abdalla Shekimweri,akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo (aliyevaa shati la rangi ya zambarau)katika kituo cha Mwakanga wakati wa majaribio ya mabehewa matatu ya TAZARA yatakayotumika kwa Usafiri wa Dar es Salaam jana.Mabehewa hayo yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria 80 waliokaa kwenye Siti na yanatarajiwa kuanza kufanya safari zake kati ya Dar es Salaam-Mwakanga na Dar es Salaam-Kurasini kuanzia mwezi Oktoba Mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Mimi naona hayo mabehewa ni makubwa sana. Zaidi ya kuchukua watu wa kukaa yanaweza kuchukua watu wa kusimama pia. Na kwa kufanya hivi ndio watakuwa wamechangia kupunguza tatizo la usafiri jijini. Ili watu waweze kusimama inabidi kuwa na nguzo na sehemu za kushikia humo ndani ya behewa. Hivyo nawashauri wahusika kuweka nguzo na sehemu za kushikia ndani ya hayo mabehewa.

    -Mdau ughaibuni

    ReplyDelete
  2. Safi sana Serekali.Mungu akujalie mafanikio mema Mh Mwakyembe na wote waliofanikisha. Uwezo tunao nguvu tunazo.

    ReplyDelete
  3. Kina Mh MwaKyembe na Mzee Kilima Hongereni vitu kama hivi Wa-Tanzania wengi walivisubiria Mdau juu hapo nafikiri wakusimama pia watakuwepo kwa idadi ya Usalama ushauri wako mzuri kuweka vyuma vya kuweza kushikia. Umuhimu tu na sie Wananchi tusiweke uchafu na vitu vya hatari kwenye njia za Reli.

    ReplyDelete

  4. Something is better than nothing
    hongereni sana lakini sasa imefika wakati wa kuwapeleka wale Tanzania One germany wakasome jinsi ya kufunga magnetic trains kama huku Japani itakua nzuri sana kuliko hizo zilizopo zinatumia petrol/diesel

    ReplyDelete
  5. MADIASPORA MAJUU KARIBUNI BONGO!

    Mnaona nyingine hiyooo?

    Kwisa faham?......kila kitu chini ya jua Bongo Tambarare!!!

    1.Reli ya Kati usafiri Jijini kama kawa.

    2.Mabasi yaendayo kasi yapo njiani.

    3.Reli ya Uhuru Jijini nayo ndiyo hiyo.

    Je kuna sababu ya kuendelea kupanda Matreni waliyojengewa wenzenu na Serikali zao huku wakiwa nyanyasa huko kwao?

    ReplyDelete
  6. Ohhh sisi haturudi Tanzania Jijini Darisalama pana shida ya usafiri!.

    Mimi hapa Mjini Boston naishi kwa raha na kufanya kazi Chicago naenda kazini kila siku na kurudi.

    Haya sasa Matreni na sisi tunayo ndio hayooo!

    Acha kazi ya kubeba maboxi Chicago na ondoka Boston-Marekani unakoishi uje Bongo tukupe kazi Ofisi ya Maliasili Mpiji au Gendagenda Mkoa wa Pwani utakuwa anakaa Dar Es Salaam na kuwahi kazini kwenda na kurudi KWA TRENI KILA SIKU !

    SAWA MAGANGA?

    ReplyDelete
  7. Hongera kwa jitihada za Usafiri!

    Ila waksafiri wa Dar msije mkaanza kuchora machata ktk viti na kuta za Treni!

    ReplyDelete
  8. Jamaa samahani huyu jamaa anayekazana na jamaa wa ughaibuni warudi nyumbani. Hivi wewe una akili timamu? Unaonekana mwehu kwangu. Acha hizo. Auna point.

    ReplyDelete
  9. Mdau wa Mon Oct 01, 04:41:00 PM 2012

    ..Acha hizo.Auna point.

    Wewe ndio mwehu !

    WATU KAMA WEWE NDIO NYIE MADIASPORA MNAOKWAMA NJE YA NCHI LAKINI MNAKUWA WAGUMU KUPATA UJASIRI WA KUREJEA NYUMBANI!

    KUMBUKA ZIZI LA NG'OMBE LINA KINYESI KIMEJAA LAKINI CHA AJABU NG'OMBE AKIVUNJIKA MGUU NI KAWAIDA YAKE KUREJEA ZIZINI AKAINGIA NDANI HATA KAMA MUDA UNGALI NI MAPEMA SIO JIONI SAA ZA KURUDI ZIZINI !!!

    KAMA WEWE UPO BONGO, INAONYESHA HUNA MICHONGO YA PESA NDIO MAANA UNAJENGA IMANI KUWA KUKAA NJE YA NCHI NDIO KUFANIKIWA!

    PIA INAONYESHA HUFUATILII MAMBO NA MABADILIKO YA MAISHA NA KIUCHUMI DUNIANI, HUWEZI AMINI PANA WAZUNGU KUTOKA NCHI KAMA URENO, SPAIN, UGIRIKI, ITALY,SPAIN NA ZINGINE WANAHAMA KWAO WANAKUJA AFRIKA KUWEKA MAKAZI YA KUDUMU...WEWE HUNA TAARIFA UPO KIZANI ULAYA IMESHA FILISIKA KIFEDHA NA KIUCHUMI NDIO MAANA HATA WAZUNGU WANAHAMA KWAO KUJA AFRIKA.

    MAJUU HAKUNA SERA, WATU WANAVUJA JASHO KWA KUBEBESHWA MABOKSI !!!

    KALAGA BAHO!!!

    ReplyDelete
  10. We Anonymous said...
    Mdau wa Mon Oct 01, 04:41:00 PM 2012
    Unachufua hewa tu. Mtu wa Ughaibuni aliyekuuzi malizana naye huko huko. Kama si wewe usiebeba maboksi, kinakuuuma nini? Unakisia tu, watu wako hivi au vile. Wacha kujenga chuki binafsi. Mtu arudi asirudi ni upendo wake mwenyewe kufuatana na nafsi yake. Wewe wala si mie atuko bora zaidi ya mwingine, kwani mwishoni wetu ni mauti tu. Wacha kujifanya we zaidi ya wezanko. Naomba Mungu akupe welevu uone vyema.

    ReplyDelete
  11. We we mmatumbi point less.tulia bongo huko, domo lako kuuubwa

    ReplyDelete
  12. Mon Oct 01, 09:20:00 PM 2012

    Mon Oct 01, 11:09:00 PM 2012

    Ninyi wabeba mabox wawili hapo juu Mnatakiwa mrudi Bongo mje kushiriki kukimbiza Mwenge wa Uhuru kuanzia Dodoma hadi Shinyanga unakozimwa mwaka huu.

    Baada ya Mbio za Mwenge tunawakabidhi Vijijini muanze Kilimo cha Kisasa hivyo mtaweza kuhamisha Teknolojia ya Kilimo bora kutoka Majuu hadi Tanzania na kuleta kasi ya maendeleo itakayokuwa Uchumi nchini Tanzania.

    Sasa nani wa kutegemwa kama sio ninyi?, hamjui ya kuwa mjenga nchi ni Mwananchi na mvunja nchi ni huyo huyo Mwananchi?

    Hivyo ndio njia pekee ya kuamsha ari yenu ya Utaifa na Uzalendo ambayo imeshapotea na sasa mnabaki Kuilalamikia Serikali, Chama Tawala na Nchi yetu nzuri ya ahadi Tanzania!

    WIMBO:

    TANZANIA ,TANZANIA
    NAKUPENDA KWA MOYO WOTE X 3

    NCHI NZURI TANZANIA
    JINA LAKO NI TAMU SANA X 3

    ...(repeat CORRUSS)

    ReplyDelete
  13. Ninyi watetea Majuu :

    Mjitahidi kuelimika !

    Nchi kama Tanzania inaweza kujengwa kwa watu wake kufanya kazi za ubebaji wa Maboxi nchi zingine?

    Hiyo hela ya ubebaji wa Maboxi ni Kipato chenye kumpa uwezo Muhusika (Diaspora) uwezo wa yeye kulewa Pombe Bar, kuchukua wake na wapenzi wa watu akija Bongo na kusaidia Ukoo wake pekee, siyo pesa inayoweza kusaidia kujenga Uchumi wa nchi kama Tanzania!

    Zindukeni chukueni hatua!

    ReplyDelete
  14. Mpendwe vipi ninyi wa Majuu?

    Sababu kubwa mlikuwa mnasema ,ohhh Bongo sirudi usafiri mgumu kuanzia Mijini na Vijijini...Ohhh huku Majuu tuna Ma-Treni ya Umeme mimi nakaa kama Tabora nafanya kazi Darisalama na nawahi kazini na kurudi nyumbani kila siku!

    Sasa mambo mswano Usafiri wa Ma-Treni kwa Pesa za Serikali hadi Mijini kama hivi mnaona hapo!

    Miaka nenda miaka rudi watu wa Darisalama hasa wakazi wa Mbagala, Tegeta na Gongo la Mboto tumekuwa tukipandia mabasi ya Toyota-DCM kwa kuingilia madirishani,,,sasa Ukombozi umepatikana!

    Kwa nini msifunge mizigo mrudi nyumabni?

    Sasa mpendwe vipi Mwanawane?

    ReplyDelete
  15. Wewe unapoikimbia nchi yako je?

    1.Matatizo ya nchi atatatua nani?

    2.Je kama wewe unakimbia nchini nani aongoze nchini?,

    3.Kwa nini unakimbia nchi halafu huko mbali maili 10,000 unabakia kutoa lawama dhidi ya Serikali na Chama?

    4.JE, PANA KABILA LOLOTE LA TANZANIA LINAO MSIMAMO WA KUWA VITA IKIZIDI WEWE ASKARI UTUPE CHINI BUNDUKI UKIMBIE?

    5.HUKO MAJUU ULIKO KWENYE MAENDELEO ,JE HAO WENYEJI WAKO WALIPIGA HATUA HIYO KWA KUIKIMBIA NCHI YAO?

    6.KAMA WALIIKIMBIA NCHI YAO WENYEJI WAKO MAJUU WEWE UNGEYAKUTA HAYO MAENDELEO UNAYOJITETEA KUWA NDIO YANAFANYA UKAE HUKO?

    KUIKIMBIA NCHI YAKO HUO NI UJASIRI WA KUTOKA KABILA GANI NCHINI TANZANIA?

    ELEWA, CHALLENGE IS KEY TO DEVELOPMENT (CHANGAMOTO NI UFUNGUO WA MAENDELEO) PIA HUWEZI KUTEGEMEA MAENDELEO NCHINI KWAKO KUPATIKANA KAMA MVUA AU KAMA MIUJIZA !

    JE, HUKO ULIKO WENYEJI WAKO WANAILAUMU TANZANIA?

    7.LAWAMA ,LAWAMA ,LAWAMA TU, KAMA WEWE NDIO MTANZANIA MWENYEWE NANI ATATATUA YANAYOIKABILI NCHI YAKO?

    ReplyDelete
  16. Angalieni Madiaspora hawa !

    1.Wewe huko Majuu unajisaidia na kuoga katika Mabafu ya sakafu za kung'ara wakati wandugu zako na wazee wako Bongo wanajisaidia ktk vyoo vya PASIPOTI SIZE?

    2.Wewe huko Majuu unayo Bima ya Matibabu umelipiwa tena na Serikali ya Majuu wakati huku Bongo bandugu zako wanaenda kwa Rehema ya Mwenyezi liende liende!

    Wakati ninyi mlipokuwa Bongo kabla ya kufika huko Majuu tuliwasomesha kwa kuchoma mahindi na vitumbua huku tukisuka mikeka?

    Kweli Bi.Chausiku na wewe Bwana Bahati Majuu ni vyema hivi?

    Na hivi sasa mnatuachia maiti kwa kututelekeza kimaisha Bongo!

    Kweli huu ni utu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...