Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Upanuzi wa barabara ni mzuri kabisa natoa Hongera na nimefurahi sana kuona maendeleo mazuri huko nyumbani. Lakini pia nimeiangalia video hii kwa makini nikagundua uendeshaji wa magari ni mbovu kabisa tena ni wa hatari usalama ni mdogo sana yaani hatari ni asilimia 90, nimeona hayo madala dala yana simama kizembe kabisa bila kuonyesha signal kama indicator kama yana simama au indicator wakati yana ondoka sasa zikipanuliwa hizo barabara ajali si ndo zitazidi?? au mnalionaje hili ??? mdau Leicester. uk

    ReplyDelete
  2. bado kabisaaaa mimi sirudi huko bado niponipo kwanza

    ReplyDelete
  3. wewe mdau wa Leicester UK,kama umechoka na mabox kalale.Huku hatuongozwi na indicator bali tunatumia akili. Je una data kamili za ajali za sasa hivi wakati barabara zetu ni finyu?? na unamakisio yapi kwamba baada ya upanuzi wa hizi barabara ajali zitakuwa ngapi ????? haya tupe hizo data basi ,kwa vile wewe umesoma sana huko UK, wacha pombe ,tulia tukujengee nchi.Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  4. walengwa wa UK huyo anaitwa Shabani Patrck Balisidya ni muimbaji hatari sana wa enzi zetu.Hapa ilikuwa kuruka majoka mpaka asubuhi,kulikuwa hakuna ukimwi wala nini,ngoma ilikuwa bila viatu,halafu kulikuwa hakuna maandamano ya chama hiki wala kile,mambo yalikuwa shwaliiii,tulivuuu,kama bajeti yako mtu ni ndogo huwezi kwenda Margot au Sky ways ,basi unakwenda Kisutu,kule ilikuwa senti 50 tu.Sasa mmekuja nyie wajanja !!! mambo sasa hovyo hovyo, mara ukimwi,mara saratani mara Polisi nakadhalika. Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  5. HILO JINA LINA MAANA GANI? "MABASI YAENDAYO KASI" itakuwa kwa spidi gani? mi nafikiri ingeitwa ujenzi wa "njia ya mabasi" au njia maalumu ya mabasi ya abiria". Halafu ikishajengwa, tuone ustaarabu wa madereva kama wataiheshimu, au watatanua humohumo na kuzuia mabasi.

    ReplyDelete
  6. Safi sana, lakini sijui barabara hiyo yatoka wapi na yaenda wapi. Kisha mbona hakuna wingi wa pikipiki au tukutuku na zile basikweli za engini ya kiuno.

    ReplyDelete
  7. ------------MSAADA-------------
    Ankal mimi bwana naomba hiyo ngoma utuwekee link yake youtube au sehemu yoyote ilipo, imenikumbusha nyumbani Mbarali enzi hizo Radio Tanzania inavuma kama nyuki.
    Mdau USA

    ReplyDelete
  8. Wakatai raisi Obama aomba muda zaidi kutimiza ahadi zake ni la kufurahisha kuona Mheshimiwa Jakaya anafanya kweli licha ya kuwa hali ngumu ya uchumi duniani. Sasa ni wajibu wetu kuhakikisha kasoro ndogo ndogo tunaziweka sawa ilitufaidike ipasavyo na huu mradi. Wadau tujaribu kuleta mawazo mbadala endelevu tuwache lawama. Miundo mbinu tumeona umahiri wa JK sasa muda umefika wa kushuhulikia mafisadi, na wale wenye siasa za udini na ukabila. Mungu ibariki Tanzania yenye kudumisha umoja wa kitaifa.

    ReplyDelete

  9. MADAU AHSANTE KWA KUILETA HII HAPA, MIMI UMENIGUSA NA HICHO KIBAO CHA WEEK END, NILIKUWA NAUSIKIA WIMBO HUU NIKIWA MDOGO NA SIKUJUA UMEIMBWA NA NANI MPAKA LEO NILIPO UKUTA HAPA. BAADA YA KUONA JINA LA BALISIDYA HARAKA NIKA YOU TUBE NAKUKUTA MAMBO MAKUNWA SANA AHSANTE MDAU

    HAYO YA UPANUZI WA BARABARA MM NAONA NI RECIPE FOR ACCIDENT,HILO JINA TU MIE NAOGOPA UNAAMBIWA MABASI YAENDAYO KASI, HAYA MABASI YA BUFALLO NI MOTO MWINGI SIKUAMBII HAYO YA MWENDO KASI!

    WAONGEZE NA HOSPITALI TEULE ZA MWENDO KASI

    ReplyDelete
  10. mimi nimefurahi lakini kituo hatuja kiona hata kimoja na nimeshalalamika sana michuzi atuwekee kituo kimoja ambacho ni kipya na kingine caha zamani kama cha moroko ili tu one utofauti maana maana nimeona ka kituo kama kamewekwa kama kibanda cha mlinzi na kipo barabarani.tuonyeshe please.

    ReplyDelete
  11. wasisahau kuweka vibao vya speed limit katika barabara sio watu waendeshe kwa makisio tuu,ni kweli kuendesha lazma utumie akili ila sio kwa style hiyo utajuaje km mwenzako wa mbele anataka kuingia barabarani bila yasignal jmn nyumbani tuache mtindio wa akili tuamke sasa ni aibu nakwambia wewe mdau wa hapo juu,license zenyewe zinatoka kimchongo kweli ajali zitapungua serikali na mamlaka za usafirishaji zinatakiwa kuwa mamcho kwa mambo ya bararani kwakweli ni aibu.

    ReplyDelete
  12. wewe zebedayo ndio utakuwa umedata zamani maneno niliyosema mimi yote ni ya kweli waulze watu wenye kujua usalama wa barabarani utaafamishwa. wewe unaonekana katika hao wazembe!! wewe kuanzia leo jina lako ni KICHWA CHA MWENDAWAZIMU!!! mdau Leicester.uk.

    ReplyDelete
  13. Na ninyi wenzangu ambao tuko majuu wote jamani tuweni na shukrani angalau kwa wenzetu walioko huko maana sisi tulikimbia wao wameamua ku-deal na matatizo ya nchi yetu. Sisi tulishindwa tukakimbilia nchi zilizoendelea bila kujua kuwa hata hawa wenzetu ilibidi wapitie kikombe hicho hicho kufikia walipo. Sasa badala ya kukaa kulaumu lazima tujiulize mchango wetu ni nini zaidi ya kulalamika? Mimi naona haya ni maendeleo japo kunatakiwa kuwe na vituo maalum vya mabasi na yasiruhusiwe kusimama kiholela. Pia kuna haja ya kugawa hizo barabara na mstari wa katikati ili kupunguza ajali. Ni maoni si malalamishi...!! Mdau, CA-USA

    ReplyDelete
  14. wewe mdau wa CA USA na wewe acha zako za kukoroga, sawa umetusifia na kuwakanya hao wabeba mabox wenzako lakini, umeharibu kwa kusema eti ,ziwekwe alama na hiki na kile , jamani !! kwani unafikiri sisi huku ni mbumbumbu ?? kuna mainjinia wazuri kushinda hao wa huko wenye vyeti vya asosieti degree,ukimuuliza 2x2 anatafuta kakuleta. hey yo listen yo, hizo alama zitawekwa na mengine mengi tu.Njoo mwakani kutembea kama hutaamua kubaki.Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  15. Hivi nyie wadau mnaojiita wa ughaibuni aka wabeba mabox mbona mnaringa sana wakati mpo kwa watu na sio kwenu? Alafu kwani ni lazina tujue upo ughaibuni? Acheni ulimbukeni nyie! Ukiona tatizo shauri kwa kutoa mifano halisi ya ulipotembelea. Am proud to be a Tanzanian

    ReplyDelete
  16. Wewe zebedayo nimekushtukia unawachukia watu wa ughaibuni(wabeba box) sasa sijui wamekufanya nini au wamekuchukulia mkeo??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...