Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dr. Hussein Mwinyi akifungua mkutano wa mwaka wa siku nne wa wataalamu kutoka nchi za Afrika Mashariki na wafadhili kwenye mapambano dhidi ya Malaria uliofanyika leo mjini Arusha.
Wajumbe wakiwa makini kufatilia hotuba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dk Hussein Mwinyi wakati akifungua mkutano wa wataalamu wa afya kutoka nchi za Afrika Mashariki na wafadhili walio kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria mjini Arusha.
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii,Dr Hussein Mwinyi(kulia)akizungumza na viongozi wa taasisi ya Eastern Africa Sub-Regional Network(EARN)kwenye mkutano wa wataalamu wa afya dhidi ya ugonjwa wa Malaria unaofanyika mjini Arusha leo.

Waziri wa Afya na Ustawi Jamii,Dr Hussein Mwinyi amezitaka nchi za Afrika kutenga kiasi cha fedha kwaajili ya kupambana na ugonjwa wa Malaria badala ya kutegemea wafadhili ambao wamekuwa wakipunza kiasi cha fedha wanachoto kila mara.

Dr Mwinyi ametoa kauli wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Mameneja wa mpango dhidi ya maambukizi ya magonjwa ya Malaria kutoka nchi 13 zilizopo Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Alisema changamoto inayokabili mapambano dhidi ya Malaria ni utegemezi wa fedha za wafadhili ambazo sio endelevu.Hata hivyo alisema Tanzania imepunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano kwa asilimia 75.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mbona kila kitu Arusha au sababu mkimaliza mnaenda kutalii mbugani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...