Mshindi wa Redd's Miss Talent 2012,Babylove Kalala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na warembo wengine walioingia hatua ya tano bora ya Redd's Talent iliyofanyika usiku huu katika hoteli ya Giraffe,jijini Dar es salaam.Kutoka kulia ni Mshiriki namba 13 kutoka kanda ya Mashariki,Joyce Baluhi,Mshiriki namba 15 kutoka Temeke,Catherine Masumbigana,Mshiriki kutoka Kanda ya Mashariki,Irene Verda na Mshiriki namba 26 kutoka Kinondoni,Brigit Alfred.
Mgeni Rasmi katika Onyesho la Redd's Miss Talent,Mbunge wa Viti Maalum - Arusha,Mh. Catherine Magige (katikati) akizungumza machache wakati akifungua shoo hiyo inayofanyika hivi sasa katika Hoteli ya Giraffe,Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa Rino International Agency ambao ni waandaaji wa Mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya Giraffe,Dk. Charles Bekon.
 Mshindi wa Redd's Miss Talent 2012,Babylove Kalala akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma za asili kwa kutimia Nyoka.

 Mshiriki namba 27 kutoka Ilala,Noela Michael akionyesha kipaji chake cha kuimba.
 Mshiriki namba 8 kutoka Kanda ya Ziwa,Happyness Rweyemamu akionyesha kipaji chake cha kuruka sarakasi katika onyesho la kumpata mrembo mwenye kipaji linaloendelea hivi sasa katika Hoteli ya Giraffe,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam usiku huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...