Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Salome Sijaona akimkaribisha rasmi Waziri wa Fedha pamoja na ujumbe kutoka Tanzania kwa chakula cha usiku alichowaandia. kutoka kulia ni Mhe. William Mgimwa Waziri wa Fedha akifuatiwa na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe. Omary Yusuph Mzee akifuatiwa na Bw.Selivicius Likwilile Naibu Katibu Mkuu Wizara na Fedha na wengineo ni viongozi waliohudhuria hafla hiyo Jijini Tokyo – Japan.
Waziri wa Fedha Mhe.
William Mgimwa akimshukuru Mhe. Balozi Salome Sijaona pamoja na mume wake
Mzee Sijaona (aliye upande wa kulia kwa Mhe. Balozi Salome Sijaona) kwa mwaliko wa
chakula cha usiku.
Wajumbe wa mkutano wa IMF na WB wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Salome Sijaona alipokuwa anatoa historia fupi ya ubalozi wa Tanzania.
Wajumbe wa mkutano wa IMF na WB wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Salome Sijaona alipokuwa anatoa historia fupi ya ubalozi wa Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Salome Sijaona akimwelezea Waziri wa Fedha Mhe William Mgimwa mambo muhimu ambayo yanapaswa kufanyika katika Balozi zetu.
Afisa wa ubalozi Bi Agnes akiwakaribisha wageni chakula cha usiku hapo ubalozini jijini Tokyo Japan.
Wajumbe kutoka Tanzania wakishiriki chakula cha jioni pamoja na Balozi Mhe. Salome sijaona.
hongera nyingi. vurugu zimetulia huko twatumai
ReplyDeleteMh.Mgimwa anauziwa toyota
ReplyDelete