Mkurugenzi wa Masoko na Utafika wa benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika tafrija iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa PPF jijini Arusha hivi karibuni.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa PPF,Dk. Adorf Mkenda (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Benki ya CRDB wakati wa hafla ya Mkutano Mkuu wa PPF uliomalizika jijini Arusha hivi karibuni. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Utafika wa benki ya CRDB, Tully Mwambapa, Mkurugenzi wa tawi la Arusha, Chiku Issa, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Saugata Bandyopandyay na Mwenyekiti wa Bodi ya benki ya CRDB, Martin Mmari. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio  akiwaongoza wageni mbalimbali kupata chakula wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika jijini Arusha kwa ajili ya wajumbe wa mkutano Mkuu wa PPF ambapo benki ya CRDB ilidhamini tafrija hiyo.
 Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Utafika wa benki ya CRDB, Tully Mwambapa, Mkurugenzi wa tawi la Arusha, Chiku Issa wakicheza Rhumba wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa wajumbe wa mkutano Mkuu wa PPF. CRDB ilidhamini hafla hiyo iliyofanyika jijini Arusha.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Saugata Bandyopandyay (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Utafika wa benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto)  na Mkurugenzi wa tawi la Arusha, Chiku Issa wakati wa hafla hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...