MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIA (IGP) SAID.A.MWEMA AKITOA TAARIFA YA KIFO CHA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI (ACP) LIBERATUS BARLOW KILICHOSABABISHWA NA KUPIGWA RISASI ENEO LA KITANGIRI MKOANI MWANZA. KULIA NI KAMISHINA WA OPERESHENI WA JESHI LA POLISI CP. PAUL CHAGONJA.( PICHA NA OFISI YA MSEMAJI WA POLISI.)

Napenda kutumia fursa hii kuwapa taarifa kuhusu tukio la mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishina Msaidizi wa Polisi Liberatus Barlow yaliyofanywa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi usiku wa kuamkia leo tarehe 13/10/2012 majira ya saa saba usiku Mkoani Mwanza. 

Tukio hilo limetokea wakati kamanda huyo akitokea kwenye kikao cha harusi ya ndugu yake eneo la Frolida hotel Mwanza mjini, akiwa na ndugu yake waliyeongozana nae kutoka kwenye kikao hicho. 

Wakati akimshusha huyo ndugu yake eneo la Kitangiri Minazi Mitatu, walitokea watu wanaosadikika kuwa ni majambazi, na kumvamia na kuanza kumshambulia kwa risasi na kumuua papohapo.

 Ndugu wananchi, kufuatia tukio hilo, tayari nimemtuma Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI Robert Manumba kwenda mkoani Mwanza kwa lengo la kuimarisha ulinzi na upepelezi wa tukio hilo.

Najua tukio hili limetushitua na kutuhuzunisha wote. Hivyo, wakati tukiendelea na taratibu zingine kuhusiana na tukio hilo, niwaombe wananchi wote kuwa watulivu na kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi, utakaowezesha kuwabaini wahalifu hao.

 Tutaendelea kuwapa taarifa za tukio hilo, kadri tutakavyoendelea kuzipata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Poleni na msiba. Waliondoka na mali zozote? Majambazi huwa wanataka kutwaa mali. Kama walimpiga risasi bila kuchukua mali yoyote walikuwa na sababu tofauti za kumshambulia.

    ReplyDelete
  2. Bwana Mwema,kwanza pole na kifo hiki,pole pia kwa Familia ya marehemu.Pili,kufanyike utaratibu wa kuwapa ulinzi hawa Ma-RPC/hata ma-OCD kwa sababu 'nature' ya kazi zao kwa namna moja au nyingine zinawasabishia maadui wengi uraiani.Sitaki kuingilia uchunguzi wenu lakini hapo nahisi ni mambo ya kulipiza kisasi.Ni maoni yangu tu

    David V

    ReplyDelete
  3. hivi we david v unapatikana wapi ukiachilia mbali kwenye blogu ya michuzi?

    ReplyDelete
  4. Polisi imeoza siku nyingi ni dawa yake ni kuisafisha. Huyu RPC alikuwa na mambo yasiyokuwa na maelezo. Saa hizo, yuko na mwanamke asiyejulikana, anazurura mitaani mara sijui anatoka baa, kweli hayo ni maadili ya kamanda mzima? Alimwacha wapi mlinzi wake na kwa nini asiwe na dereva saa kama hizo au kwa nini asipelekwe nyumbani na kumwacha huyo dada apelekwe na madereva wake? Ni suala la maadili tu hapa, na hii ni dalili kwamba kuna shida nyingi Polisi na sasa zinatoka hadharani. Polisi yetu inahitaji mabadiliko kama ilivyo kwa serikali pia.

    ReplyDelete
  5. Mdau mimi hapo juu nipo bwana humu duniani napambana na maisha ndugu yangu .Nitafute hapa atyini@yahoo.com karibu sana kiongozi.!

    David V

    ReplyDelete
  6. Nashangaa sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...