Kiongozi wa jumuiya ya Uamsho, Ustaadh Farid, akiwa na nduguze baada ya kupatikana akiwa katika hali nzuri na kwa sasa yupo kwao kwa mzazi wake Unguja  akipumzika.
Ustaadh Farid akiwa na familia yake mara baada ya kupatikana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Assalam Alaykum Sheikh?

    Uhali gani?

    Ulikuwa wapi Sheikh siku zote hizi?

    Hebu tupe kwa uchache!

    ReplyDelete
  2. Nyerere Angekuwa ana Nguvu zaid, angeunganisha Africa nzima na sasa wote tungekuwa hatulilii shida.

    Kwa Wasilamu Wenzangu :

    DO NOT BE FOOLS / TUSIWE WAPUUZI WA KUPELEKWA WANAPOTAKA WANSIASA.

    Ushauri wa Bure : HUYU SHEHE ANAPIGANIA SIASA NA SIO UISLAMU (Quote: Amesema mwenyewe kwamba anataka Zanzibar Huru kwa maneno mengine - HATAKI MUUNGANO).

    Sasa kama wewe ni musilamu na sio mwanasiasa, ninakuomba umuache yeye na hao wanasiasa wenzie kwani wao wanatufuta liberation ya kwao ila wanatumia NGUVU YA WAISLAMU kutimiza matakwa yao.

    Mimi nilitegemea kuwa angesema Serikali ya Zanzibar inataka kubomoa misikiti yote, hivyo tunataka kupigiania nyumba za mungu, kumbe anataka uraisi oh sorry Zanzibar huru ... mhmhmh (joking).

    HAYA MANENO YA KUAMBIWA CHANGANYA NA AKILI YAKO.

    ReplyDelete
  3. Sasa atueleze alikuwa wapi sio kusingizia serikali muungano upo palepale asijidanganye

    ReplyDelete
  4. Sawa tumemsikia Ustaadh,madai yake yapo ya maana kama vile kuwataka wananchi waache vurugu,yeye amesema maetekwa lakini wanausalama wanakanusha kuhusika,inawezekana ukawa mchezo wa kuigiza hili kupata chanzo cha fujo,(B) anapodai uhuru wa Zanzibar liwe taifa uhuru anamaana gani? yaani muungano uvunjwe? sasa kama swala la muungano ni swala la makubaliano ya pande mbili bara na visiwani,sio bara tu.
    Tanzania bara haijavifanya visiwa vya unguja na pemba kuwa koloni hata siku moja,kama ni kuvunja muungano ni swala la kukaa mezani kulijadili sio kwa fujo.
    Sheikh katika maelezo yake anasema kaelezwa mengi toka aachiwe uhuru mbona hajagusia kuhusu kifo cha askari wa FFU ! inamaana kitendo ha kuuwawa askari huyo ndio kukamilisha usemi wa Sheikh kuwa Zanzibar ataitetea hata kwa tone la damu la mwisho ?
    Waislamu tusikubali kugawanya na vibaraka wa maghaidi kwa kuvunja amani kwa kisingizio cha dini

    ReplyDelete
  5. AH! Tumemsikiliza sheikh,lakini madai yake ya kutekwa hayana uhakika,mpaka upande unashutumiwa nao utoe maelezo.
    Lingine ambalo wengi labda tutamuona sheikh ni mnafiki pale anapodai anataka Zanzibar liwe taifa au dola huru kama lilivyokua mwaka 1963 ! hivi anamaana gani ?yaani utawala wa waarabu urudi? kama ilivyokua kabla ya mapinduzi 1964 kwa maana Zanzibar katika uchaguzi wa mwaka 1963 ulikua utawala wa sultan bado una mamlaka
    sasa ustaadhi anapodai Zanzibar irudi kama ilivyokua 1963 watu hatumwelewi ana maana gani? mfumo wa kisultani urudi upya au?
    Waislam Tusikubali kuchanganywa akili wa baadhi ya watu wasiopenda amani

    ReplyDelete
  6. angalia wasikukamate tena kikweli kweli ohoo shauri yako wana usongo sana na wewe mkuu shauri yako tahadhar sana na nenda kapime wasije wakawa wamekuwekea sumu katika kile kitaamba walicho kufunika nacho

    kila la kheri mkuu

    ReplyDelete
  7. uamsho mbona yeye kalala????

    ReplyDelete
  8. NAOMBA KUULIZWA KWANI UKILAZIMISHA NDOA MADHARA YAKE NINI????

    ReplyDelete
  9. kamguse uone kama kalala atakushughulikia vilivyo kuliko unavyo jua na unacheza na simba mwenda pole weeee

    ReplyDelete
  10. Zanzibar ilikuwa huru kabla ya hiyo 63,angalia historia ya zanzibar kama hufahamu tafuta nakala ya Periplus of erethian sea,utakuta nini Zanzibar kabla hata ya hiyo TANGANYIKA.
    AKIWA MKWELI AU SIO KWELI MSITUTOE KWENYE MADA MPANGO UPO PALE PALE ZANZIBAR KWANZA,
    MAWAZO YAKO FINYU YA KULETA WAARABU WATU HAWAYAKUBALI SASA

    ReplyDelete
  11. Mh! wazanzibari wana mambo? sasa yeye ni shehe au mwanasiasa? bora akagombee kiti cha siasa tumjue yupo upande gani? au atuambie nani kamtuma!

    Kwa mtazamo wangu, huu ni UPUUZI MTUPU. Serikali iwashughulikie hawa, BASI.

    ReplyDelete
  12. Dr.Steven Ulimboka amesema katekwa kila mtu anasema KWELI AMETEKWA

    sheikh Farid anasema ametekwa kila mtu anasema MUONGO HAJATEKWA.

    nchi ya ajabu tunayoishi.lazima tukubali UNAFIKI tulionao.kama raia tunaoipenda nchi yetu kwa dhati kwanza tuache ushabiki.

    pili,tunaposema tunataka amani ya nchi yetu idumu serikali inatakiwa iwe tayari kutatua dukuduku na kuondoa manung'uniko ya raia wa nchi hii bila kutumia nguvu.
    Tanzania yenye watu zaidi ya milioni arobaini(40,000,000) hatuwezi kushindwa kupata jopo la watu hamsini (50) tu wenye hekima,wanaona mbali na wanaoweza kusoma alama za nyakati wakatuondolea kero zinazotukabili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...