Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma leo kwa ajili ya kufungua mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika sambamba na uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT Taifa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa akifungua mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma, sambamba na uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT Taifa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisalimiana na Mama Fatma Karume wakati wa mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya ya
Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika leo katika ukumbi
wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma, sambamba na uchaguzi wa Mwenyekiti wa
UWT Taifa.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania, (UWT) Taifa, anayemaliza muda wake, Sophia Simba, (katikati) na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa wakifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika leo, sambamba na uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT Taifa.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania, (UWT) Taifa, anayemaliza muda wake, Sophia Simba, wakati wa ufunguzi wa mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika leo, sambamba na uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT Taifa.
Baadhi ya wake wa Viongozi, wakiwa ukumbini humo wakati wa ufunguzi huo wa mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika leo, sambamba na uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT Taifa. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...