Mwenyekiti mpya wa UWT Sophia Simba akipongezwa na mke wa Rais wa Zanzibar mama Mwanamwema Shein baada ya kuibuka mshindi kwenye uchaguzi wa UWT jana usiku.
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akitowa nasaha zake kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma na kumchangua Mwenyekiti Mpya Sophia Simba.
MWENYEKITI wa UWT Mhe. Sophia Simba na Makamu wake Mwenyekiti Mhe.Asha Bakari Khamis, wakiwa na furaha baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi mkuu wa umoja huo uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha mpiango dodoma.
VIONGOZI wa meza kuu wakishangilia baada ya kuitolewa matokeo ya kura za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa UWT, baada ya uchaguzi kufanyika kuwachagua Viongozi hao.
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa UWT wakishangilia bbaada ya kutangazwa jina la Mwenyekiti mpya wa Umoja huo Mhe. Sophia Simba na Makamu wake Asha Bakari katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma jana usiku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera sana Mh Sophia Mnyambi Simba, UWT itaendelea kuwa imara. Tunataka viongozi CCM damu na si CCM-Maslahi

    ReplyDelete
  2. Hii Sasa ni umoja wa wanawake wa Tanzania au umoja wa wanawake wa CCM? I think they should change the Name to UWCCM na warudishe mali zote za wanawake wa Tanzania. Chama kichague upya viongozi wake na wanachama wapya wakiwemo wa vyama vingine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...