Kuna taarifa kwenye mitandao ya simu inayoendelea kutolewa kwenye message za simu kwamba  kuna Mabomu zaidi ya 30 yenye uzito usiopungua tani 100 na kuwataka wananchi katika mikoa ya Tanzania iliyo jirani na Malawi kuwa waangalifu. 
 
Taarifa hiyo imetaka wenye wasiwasi kuhusu taarifa hiyo wapige simu 0756000042. Taarifa hiyo imedai kwamba imetolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Tunapenda kutoa taarifa kwamba taarifa hizo siyo za kweli na lengo lake  haliwezi kuwa zuri kwa Watanzania.  Wananchi wanashauriwa kutotuma taarifa zozote kwenye namba hiyo ama kuziamini taarifa za aina hiyo.


Assah Mwambene
Mkurugenzi, Idara ya Habari Maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hawa wanajeshi wanaozurura,kuchoma mafuta mitaani na kupiga trafiki wachunguze sasa ukweli wa hizi taarifa ili kuondoa hofu kwa wananchi na sio kuleta ubabe mbuzi mjini hapa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...