Habari ya asubuhi kaka Issa, 
Samahani naomba uniwekee tangazo nimedondosha wallet yangu katika basi la mwananyamala stesheni asubuhi wakati nakuja kazini.
Naomba mtu yeyote atakae ona vitambulisho vyangu tafadhari anidondoshee hapa TRA makao makuu au anipigie simu namba 0713296053  naitwa mathias Chanila. Wallet ilikuwa navitambulisho vyangu vyote
regards
Asanteni


 
Sasa wewe Bosi Mzima na Vitambulisho nyeti kama hivyo wa Saccos kama TRA ungali unatumia usafiri mbovu wa mabasi?
ReplyDeleteAu ndio kujificha ya kuwa wewe sio mlaji Rushwa na unapanda Mabasi?
Au ndio ubahili uliopindukia hata kununua Vitz inakuwa ngumu?
Inaeleweka hata Mesenja wa ndani ya Mamlaka yenye 'Ulaji' kama TRA hawezi kukosa hata uwezo wa kununua Pikipiki ya kuendea kazini!
Au ndio umekuwa Nyerere na wewe?
ReplyDeleteWenzio ktk TRA wanamiliki magarti huku wakiwa Vijogoo kwa kununulia magari vimada na kuwajengea majumba wewe ungali unapanda mabasi!
Au ndio 'babu' alivyokushauri kutumia usafiri wa mabasi sio?
Ubahili mwingine jamani??
ReplyDeleteKwa nini ukienda kazini usikodi Teksi?
Wewe unaingiza hela kibao pale TRA lakini bado unatumia mabasi!
Ahhh!
ReplyDeleteSio bure hii wewe Afisa wa Mamlaka.
Ukizidisha kufuata mshariti sana ya Wataalamu ndio kama hapa yanakukuta sasa.
Yaani unafanyakazi kwa miaka kibao na kuwa na cheo ktk Mamlaka kama hiyo yenye wizi na rushwa kupita maelezo halafu bado unapanda mabasi?
Mbona wenzio kila mmoja ana usafiri wake?
Ahhh!
ReplyDeleteSio bure hii wewe Afisa wa Mamlaka.
Ukizidisha kufuata mshariti sana ya Wataalamu ndio kama hapa yanakukuta sasa.
Yaani unafanyakazi kwa miaka kibao na kuwa na cheo ktk Mamlaka kama hiyo yenye wizi na rushwa kupita maelezo halafu bado unapanda mabasi?
Mbona wenzio kila mmoja ana usafiri wake?
Naona unataka watu wakifanyie wema wakati wewe ukiwa ofisini kwako unazingua sana watu wanaotaka huduma yako.
ReplyDeleteAnyway watanzania wavumilivu sana watakuletea tu ofisini wallet yako. Hofu ni kwamba kabla hajakueleza amekuja kufanya nini ofisini kwako unaweza kuanza kumkoromea au kumdai rushwa wakati amekuletea waleti wako. Maana wabongo mkiwa kazini au ofisini kwenu hamjali wala kuthamini watu
Wewe Mathias Chanila au unafanya Igizo la wasifu wa Kambarage Nyerere kwenye wiki hii ya maadhimisho ya kifo chake?
ReplyDeleteYaani wengi hatukuelewi kabisa humu Jamvini ukiwa ni Afisa wa TRA tunayoijua ilivyokomaa kwa rushwa , wizi na ufisadi halafu wewe ukashindwa hata kuwa na Bajaj ya kuendea kazini?
Kama ni Igizo la wasifu wa Nyerere, huna mpinzani ni wazi utakuwa umeshinda!
Afisa wa tra huyo sheikh au dakitari wako anakushauri vibaya!
ReplyDeleteKwa ubahili huu ulio nao kushindwa hata kukopa kazini uwe na usafiri wako ukawa unapanda mabasi.
Yaani TIN, Leseni za Magari na VAT nazotupiga hela ndefu mkiwa sambamba na wale vijana wenu vishoka umeshindwa hata kununua Toyo ama Bajaj kuwendea kazini kwako?
ReplyDeleteBosi wa TRA,
ReplyDeleteYaani vishoka vyote vile mnavyotupiga unashindwa hata kukodi taksi kwendea kazini?
Bosi TRA dahhh!
ReplyDeleteUna tambiko gumu sana la kutopanda gari la peke yako unaona sasa yamekukuta?
TRA ....na bado unapanda daladala sasa utaibiwa wewe
ReplyDeleteBwana Mathias Chanila,
ReplyDeleteHuyo 'Dakitari' wako mwambie akupunguzie mashariti ya kisayansi ambayo hayaendani na wakati kabisa kulingana na sehemu yako ya kazi TRA panapojulikana pana mapesa!
Kukwambia mashariti ya kuwa daima utumie 'usafiri wa Halaiki' amekubana sana na ndio maana yote haya yanakukuta wakati uwezo unao hata kwa kukopa ukawa na gari lako badala ya kupanda mabasi!
acheni kuwafikiria wenzenu vibaya jamani. kuweeni wastarabu. mtu hamumjui. sengine mfagiaji au mtu wakawaida. WATANZANIA KUWENI WASTARABU MIWE WANGA WAMCHANA.
ReplyDeleteAnkal naomba urudishe ile article fulani aliandika mdau kuhusu tabia zetu sisi watanzania.
ReplyDeleteMtanzania......
Mtanzania......
Mtanzania.....
David V
duh naona wabongo mna hasira na watu wa TRA. Sion hata anayempa pole huyu mtu aliyepotelewa.
ReplyDeleteKama kweli anafanyia TRA basi somo amelipata.
Kwa hali hii ni dalili kuwa kuna chuki kubwa sana kati ya mwenye kazi nzuri (au mwenye nacho) na asiye na kazi nzuri/asiye na kazi kabisa(asiyenacho. Na hii hali ni hatari kwa mstakabali wa amani na taifa letu.
Nimekukubali David V, nimegundua ufisadi hauwezi isha kama kila comment inamwona jamaa wa TRA bwege kwa kukosa usafiri kumbe kila mmoja akipata madaraka atachakachua tu
ReplyDelete