Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Kikwete amemteua Prof. Mwajabu Possi (wa pili kushoto) kutoka
chuo kikuu cha Dar es salaam kuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Shirika
la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 8 Octoba,
2012.
Kufuatia uteuzi huo,
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amewateua
wajumbe mbalimbali wa bodi hiyo ambao ni Dkt Mariam Nchimbi, Gideoni Mbalase, Prof.
Elizabeth Kiondo na Balozi Kassim Mwawando.
Wajumbe wengine ni Mkurugenzi
wa Idara ya Habari -MAELEZO Assah Mwambene, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu
Salva Rweyemamu, Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO Zanzibar Yusuf Omary Chunda pamoja
na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Clement Mshana.
Wakati huo huo Waziri Mkangara
amemteua Christopher Gachuma kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo
Malya.
Aidha amewateua Pendo
Malebeja, William Erio, Richard Ndassa, Lina Kessi, Leornard Thadeo na Allen
Alex kuwa wajumbe wa bodi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...