Kiongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Shekh Farid Hadi Ahmed akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakama ya Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao yanayomkabili ikiwemo kusababisha fujo na uchochezi.
Mmoja kati ya Viongozi wa UAMSHO Shekh Azan Khalid Hamdan (43) akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakamani Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao.
Gari la Polisi la pili ambalo liliwachukuwa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walishitakiwa kwa makosa ya kufanya fujo na uchochezi likiwa linasindikizwa na magari ya Polisi kuja Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakiwa wanaimarisha usalama katika eneo la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe ambapo Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO walipelekwa kwenda kusomewa mashitaka yao.
Gari la Polisi ambalo liliwachukuwa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walishitakiwa kwa makosa ya kufanya fujo na uchochezi likiwa linawasili Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe.
Baadhi ya Wananchi walioenda Mahakamani hapo kwenda kushuhudia kesi inayowakabili Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walikosa dhamana na kurudishwa Rumande.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.


Jamani, Uislamu unatumika vibaya na hao wanaojiita masheikh. Kama wanataka siasa, wauvue huo usheikh.
ReplyDeleteYaani nyie ndugu zangu wazanzibar, mmeingiwa na nini hasa kwa kuwaona hao UAMSHO ni watu wamaana!!! Jamaani, mababu zatu walipigana vita vya kumuondoa mwarabu, haya kulikoni ninyi mnataka kuwarudisha? Mnataka kuwa koloni la mwarabu?
Hao mabwana mambo yakisha chafuka, wakimbilia UARABUNI, haya na nyie wenzangu na mie mtakimbilia wapi kama si HUKO nakokuita bara.
Msikubali kutumika, tufanye kazi kwa bidii na maarifa wandugu.
Tatizo Sio uarabu wala uhindi......achana na ukabila.enzi za ukoloni zilishapita..hapa nikila mtu anaendeshwa na akili yake.
Deletehivi siku hizi alama ya maswala ya imani ni V kumaanisha ushindi ndio MUngu anataka hivyo? Just think aloud alama anayoionyesha kiongozi wa uhamsho huyo Faridi.
ReplyDeleteNiaibu kubwa sana kwa zanzibar niliyokuwa nikiijuwa zamani na leo hii mahakama ya wilaya jengo lake kama banda la kuuzia supu ya kuku.....watu wanakwenda mbele wao bado wanakandamiza watu wasio na hatia achieni watu wawe huru na wapeni wanachotaka na nikidogo sana ..hawataki muungano kwanini muwalazimishe watu nyinyi
ReplyDeleteAlisingizia katekwa, sasa wamemteka kweupe. Ami Faridi nyoa ndevu, vua kanzu, vaa granda la blue upite mitaani kuneza sera za CUF, wasikia hivyo amii!!
ReplyDeleteSiasa imeshindwa sasa twende dini hi si aibu uislam unatueleza kuwa dini ni mfumo wa maisha-hadi kieleweke - huu ni uonevu utawatakaje dhamana ya mfanyakazi wakati keeshi imeshindwa hata kuendeshwa hakuna ushahidi kisha kuwacha rumande?
ReplyDeleteWOW - DE I JUST SEE, THE UAMSHO CHAIRMAN SHOWING CHADEMA SIGN?
ReplyDeletemdau wa mwanzo tafadhali tafadhali bwana mdogo kuwa na hekma na busara wakati wa kutoa maoni/au duku duku lako katika mtandao huu.
ReplyDeleteunafikiri sisi wajinga nyinyi ndo msiyoijui historiya yenu ya tanganyika sisi tunaijui historia yetu bwana mdogo, kama unaona waraabu ndo waliotukandamiza sisi hatuoni hivyo kwa sababu tunaijua historia yetu bwana mdogo
historia yenu ya tanganyika mmepotoshewa ndo maana utasema uliyoyasema kwa kudanganywa danganyw ana fikra za baba yenu wa taifa.
so tafadhali usitulete za kuleta tafuta historia ya kwenu ya kweli si hii hii mnayopotoshwa potoshwa.
ukisema muarabu kawatesa watu je mzungu kafanya nini na bado anafanya nini hadi hivi sasa ulimunguni kote?
kuwa muelevu wa kuchunguza mambo na kusoma soma vitabu vingi sana na kwenda shule ili uelimike zaidi siyo kuja hapa kutoa pumba zako na michuzi ndo anakupendeni watu kama nyinyi
sisi tukitoa comment zetu tunaonekana za uchochezi za kwenu za kipuzi puzi ohaa ndo za kuziweka. shame on you guys.
chadema njoeni zanzibar kwa nini watu hawa wakoseshe zamani kwa nini kama raia na wakazi wa hii nchi kwa nini
ReplyDeleteccm mwaka huku mpaka kieleweke mtakiona chenu cha mtema kuni mmesazoea kuwabutuza na kuwanyanyasa watu na kuwaona hawajasoma basi mwaka huu mme ula wa chuya na ndona la mwalimu
Sawa kama hutaki muungano si hutaki. Ni lazima uhuburi chuki, ni lazima uchome makanisa, ni lazima uwachagulie watu vinywaji kwa nguvu: hivi vyote vinahusiana vipi na muungano au kuukataa muungano?? Uamsho are a peverse and retarded lot!
ReplyDeleteWewe mdau wa kwanza mwehu kweli hujui unachosema kuwa ni ubaguzi wa rangi nyie mnaojiita watu weusi mna nini cha kujivunia, kazi kubagua waarabu then mkibaguliwa na wazungu mnapiga kelele, wanaowabagua ni wazungu mnamaliza hasira zenu kwa waarabu, kama una chuki na uislamu usiwamalizie waarabu sio waarabu wote waislamu wengine wakristu kama wewe mwehuu mkubwa.
ReplyDeleteWee mdau wa kwanza nyie ndio watu mnaochochea hizi vurugu, mnakojolea vitabu vya watu hamueshimu dini za watu wengine sasa mambo magumu mnawakimbilia waarabu hujui kama waarabu ni watu waliotoa mchango mkubwa kumuondoa mkoloni hapa Tanzania. Nenda kajifunze tena historia sijui ni babu yako gani alipigana na waarabu. Kunguru
ReplyDeleteWewe mdau wa kwanza huyo babu yako aliyepigana na waarabu kamfufue umuulize vizuri, waarabu wana mchango gani kwenye hii nchi? Hujui hata kama hii nchi haijali rangi, kabila wala dini as long as you are Tanzanian una right kama mtanzania. Kama haya mombi yako yakifuatwa basi wale black Americans wasingekuwa na Rais Mweusi huna habari, ndio maana mnaambiwa mpo nyuma sijui mpo dunia gani hiyo isiyoheshimu Mila na desturi za watu. Habithi Mkubwa
ReplyDeleteNyie wote mntania tu: Muungano haufi, hata ikibidi kufa mtu atakufa.
ReplyDeleteNyinyi watanganyika mmekaa kama Michael Jackson hamutaki kuasept kuwa nyinyi ni watanganyika tu sisi WAZANZIBARI tunajipraud kama WAZANZIBARI nyinyi mkiulizwa utasikia Mtanzania acheni kugagania MUUNGANO msilazimishe vitu be real and proud your self to who you are .GOD BLESS ZANZIBAR.
ReplyDeleteeh!eh! hawa jamaa kina Ras Makunja wapo tayari tayari na magitaa yao mkononi wanangija vianze wachezeshe muziki,Sasa wale mnaoshabikiaga anzeni muone muziki wa kina Ras makunja na magitaa yao
ReplyDeleteUamsho wanataka Sultan lazima arudi madarakani,wanadai Zinjbari ni dola la kiarabu,tena msemaji wao mmoja ni mbantu kabisa anatilia mkazo kuwa wazanzibar wote takribani ni waarabu,
ReplyDeletekweli kuchanganyikiwa kubaya
Hivi Waarabu wangekua watawala bora kwanini? yalifanyika mapimduzi 1964,
ReplyDeleteWaislamu wenzetu tumuogopeni Mungu,msichanganye dini na utamaduni wa kiarabu,
Msijitie Utumwani kwa kasumba ya kuona heti mwarabu ni mtu bora kuliko mweusi, Mwenyezi mungu kasema yule aliye bora ni yule mcha mungu wa kweli na anayetubu mbele ya mola wake,
Tena Mola wetu kasema nimekuumbeni katika makabila na mataifa hili mpate kujuana,katika viumbe wa mwenyezi mungu hakuna aliye bora hila yule anaye mcha mungu.
sasa hizi fikira za kuwa utawala wa mwarabu ulikua bora Wazanzibar tunazipata wapi?
Kina Ras Makunja(FFU) na magitaa mapya mikononi! najua hapo muziki wake sio wa mipasho bali jino kwa jino kwa yeyote atakaeanzisha fujo
ReplyDeletesasa wajamaa kina ras makunja ffu hapa kisiwani wamefikaje ? kama si wazanzibar tumeyatafuta wenyewe? kina ras makunja na magitaa yao hapa sio viwanja vyao kabisa,lakini kwa kuwa tumevianza leo tumeletewa vijana kama hawa kina ras makunja au ffu ambao chochote kila wapo tayari kukifanya.
ReplyDeleteUungwana ni vitendo tuache hizi fujo
sasa wewe unayejivunia uzanzibar umekusaidia nn acheni ulevi nyie tatizo elimu dunia yote hii inaungana ona nchi za ulaya zimeungana ona marekani state zote zimeungana na kuform nchi moja USA nyie mnajivunia na uzanzibar huo ni ulevi tu na kutokua na kazi huu muungano haufi mnajisumbua ndugu zangu ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu mtaaishia kula kichapo tu wengi mmezaliwa mmeukuta muungano na mtakufa mtauacha TANZANIA OYEEEEEEEEEEE
ReplyDeleteMnh! Ukisoma tu comment za wadau hapo juu utagundua wapi wana matatizo. Sasa nyie ndugu zetu, mbona comments zenu zimejaa hasira, kashfa na matusi. Hivi hamuwezi ku-comment mpaka mtukane? Busara gani hiyo? Mnajipambanua wenyewe mu watu wa aina gani kwa lugha mnayotumia. Kwani ukimwelimisha mtu bila kumtusi hutaeleweka? Mbona huyo anony 1 mnayemshambulia hajawatusi? Hebu jirekebisheni bwana.
ReplyDeleteEbana naona police mmoja ana Colt M-15 !
ReplyDeleteUkisema wewe mznz sio sawa maana kuna WAPEMBA na WAUNGUJA.
ReplyDeletehakuna sisi wazanzibar.!ila kuna sisi watanzania.
kingine napenda kusema tu vile,kutokana na mabadiliko ya hewa na global warming..kisiwa cha Znz kitamezwa muda sio mrefu.
kwahiyo sioni cha ajabu saaana nyinyi wapemba maana waaunguja akaa wao hawana shida.
nawakilisha.
mtoto wa tajiri.
Mimi nachoshangaa hawa wanaosema wamesoma, hasa wamesoma nini mbona nchi inarudi nyuma shule gani hizi walizosoma, kinachoendeleza nchi ni hekima na busara, ebu tuachieni zanzibar wale tusiosoma na mbaki na bara muone neema itakavo funguka kwa muda mfupi. ati Shule.... shule.... nchi miaka hamsini uozo mtupu!!!!!.
ReplyDeleteTatizo si muungano bali ni uganawanaji wa mapato ya maliasili zilizomo Tanzania. Ikiwa tanzania bara wanachukua asilimia tisini na tano na nusu za pesa za dhahabu, almasi mwaduai na gesi songosongo, zanzibar nao waachiwe wachukue asilimie tisini na tano za hela za mafuta yatakayochimbwa znz. Halafu huu mfumo wa serikali mbili ni unsustainable. Twendeni kwenye confederation arrangement. Serikali ziwe tatu. lakini, no, muungano usivunjwe, ni mutually beneficial. Dr
ReplyDeleteHii ishara ya V anayo ionesha huyu jamaa, imefanya kazi kubwa ya kumwaga damu kwenye nchi nyingi sana za Asia na Afrika, na inaendelea kuvitesa vizazi vyetu, Imeanzishwa na wenye hamu ya kuona Nchi zinazo endelea zinamwaga damu ili wapenyeze kwa lengo la kututafutia Amani kumbe wakitaka kuiba raslimali zetu. Wameiba sana kwa Gadafi, Tunisia, Kongo, Kenya na kwenyewe alama hii imemwaga damu sana, Iraq ndii usiseme tena, na nchi nyingi tu. TUTAFAKARI SANA.
ReplyDeleteWaarabu wa Zanzibar wanaochochea vurugu ni wahuni tu njaa inawasumbua hawana la kufanya, na wanzanzibar walivyokataa elimu basi wanaendeshwa kama tu kama gari bovu.
ReplyDeleteMdau wa Mon Oct 22, 11:56:00 PM 2012
ReplyDelete......Nyinyi watanganyika,,,,vitu be real and proud your self to who you are .GOD BLESS ZANZIBAR.
USIKALIE KUTI KAVU, KWANI DUNIA HAITAMBUI NCHI INAYOITWA ZANZIBAR.
WENZIO WALIOKUWA UGHAIBUNI WANAFAHAMU HILI WAO WALIKUWA WANA BISHA IKATOKEA HUMU HUMU KWENYE JAMVI WAKAJA KUKUBALI UKWELI WA KUWA HATA KAMA UTAKUWA MZANZIBARI, UTAIFA WAKO UTAJIITA HIVYO UKIWA HUKO KWENU MCHAMBA WIMA ZANZIBAR, DUNIA HAIELEWI WEWE KUWA NI RAIA WA 'JAMHURI YA ZANZIBAR' LAKINI NENDA KOTE DUNIANI NZIMA INAKUELEWA KAMA RAIA WA 'JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA' UTAKE USITAKE!!!
WAZANZIBARI WENYE AKILI KAMA DR.BILAL ,DR.SHEIN NA MAALIM SEIF SHARRIF HAMAD WANATAMBUA UMUHIMU WA MUUNGANO ILA WEWE BWEGE NA WENZIO MSIO NA AKILI HAMJUI HILI!
MUUNGANO HAUFI MTAKUFA NINYI!
Zanzibar daima hutaka ligi (bone of contention) kama wake wenza,la cuf vs ccm lilipoozwa sasa wamelianzisha jengine.
ReplyDeletemimi ni mtanganyika waacheni wazenji wajitawale sioni faida yeyote tunayipata zaidi wao ndio wanafaidika kwa sisi kujipendekeza kwao umeme wanalipa chini ya gharama halisi halafu tunawangangania tuachane nao
ReplyDelete...hakuna wazanzibari kuna wapemba na waunguja...je huyo shekh kabila gani??? swali zuri sana. wanaomshambulia mtoa comment wa kwanza kwa matusi wanaonyesha kwa jinsi gani walivyo...wanadai uhuru wa kuongea na kuchagua..sasa wao wanamtukana kwa maoni yake..ha hahaa utafahamu kuwa hapo ni elimu na busara wanayokosa na hivyo ndio maana wanakuwa rahisi kubebwa na upepo....sio lazima kujieleza au kudai haki kwa fujo..je haki ya huyo mwingine iko wapi?? wananifurahisha baada ya kupata shija wanakimbilia uingereza kwenye ustaraababu...mbona msikimbilie kuwait au saud??????
ReplyDeleteni maoni yangu tu i hope sijatukana.
Tatizo kubwa la walalahoi au wachimba chumvi au kwa lugha nyingine njaa njaa wa kitanzania chuki yao kubwa ni kwa hawa warabu na wahindi ambao asilimia kubwa ndio wanaowapa choo mjini
ReplyDeleteasilimia kubwa ya watanzania mmepata ajira kupitia kwa hao warabu na wahindi kwenye viwanda vyao maduka nk
lakini kitu cha kushangaza kuwa watanzania haohao wasio na shukurani hawachoki kuwabeza warabu na wahindi
tukiachilia mbali ajira inayopatikana kutoka kwa warabu na wahindi nchini TANZANIA
Tujiulize ni watanzania wangapi waliopata kwa hao wazungu ambao wanapenda kuwa watumwa kwao
INASIKITISHA SANA WATANZANIA WAMEKUWA NA UBAGUZI WA WAZI KABISA KWA NDUGU ZAO WARABU NA WAHINDI AMBAO NDIO WAAJIRI WAO HAPO NCHINI.
KWELI SHUKURANI YA PUNDA NI MATEKE.
NCHI ZINAUNGANA kuna mtu kasema hapo juu hilo ni jinga la mwisho je mbona hatujaungwa na nchi nyengine kama Kenya na Uganda kama kuna manufaa na huu Muungano mnaoutaka/Nchi zinaungana lakini zinabakia kuwa ni nchi huru hata ulaya uloitaja Nordic countries na nyengine nyengine sio kuwa nchi moja -Scotland haoo na sio wao tu SUDAN WELL DONE SHELI SHELI HATAKI MUUNGANO WOOTE NA MATAJIRI KWA AFRIKA
ReplyDeleteCHADEMA
ReplyDelete
ReplyDeleteHuu ni muendelezo wa The Crusade. WOTE wataachiwa hao, watch this space...
Wana hoja za msingi, nyie wengine mliokunywa maji ya fitna na propaganda iko siku mtaujua ukweli tu.