Rais wa Shirikisho la Ngumi, Taifa (BFT), Alhaji Shaban Mintanga
(pichani kati) ameachiwa huru na Mahakama Kuu baada ya kukutwa hana kesi ya
kujibu.
Mintanga alifikishwa Katika Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam
akikabiliwa na mashitaka ya kula njama na kusafirisha dawa za kulevya Julai
2008 hata hivyo aliendelea kusota ndani hadi leo alipoachiwa na mahakama hiyo.
jaji Twaib kumuachia huru mshitakiwa kwa kifungu cha sheria namba 293
(1) ya mwenendo wa makosa ya jinai.
Ilikuwa ni furaha isiyo kifani kwa ndugu na jamaa za mshitakiwa huyo
baada ya ndugu yao kusota rumande muda mrefu sasa yu huru.
Jaji Dk Fauz Twaib alisema kuwa anamuachia huru kwasababu kati ya
mashitaka mawili yaliyokuwa yakimkabili, kula njama na kusafirisha dawa za
kulevya, hakuna lililothibitishwa kutendwa na mshitakiwa.
Hakuna uthibitisho kuwa mshitakiwa alikula njama kwasababu haikutolewa
ushahidi kuwa mshitakiwa ni wapi na wakati gani alitenda kosa hilo.
Aidha jaji huyo alisema pia kuwa haikuthibitishwa mshitakiwa
alisafirisha dawa hizo kwasababu yeye hakusafiri na pia washitakiwa
waliokamatwa huko nchini Mauritius walimtaja mtu anayeitwa Mika kuwa ndiye
aliyewapa na kuwamezesha katika hoteli iliyoko Manzese hapa jijini.
Jaji Fauz alisema kuwa kama ni kuhusishwa na mashitaka hayo basi ilikuwa
ni Mika ambaye upande wa mashitaka ulidai kuwa bado unamtafuta.
Upande wa jamuhuri ulikuwa na mashahidi wane tu baada ya Jaji huyo
kuwalazimisha kufunga ushahidi, toka mwanzoni mwa mwaka huu kesi hiyo ilikuwa
ikiahirishwa tu kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kuleta mashahidi
wengine mahakamani katika wakidai kuwa mashahidi hao muhimu wako Mauritius
ambao ni wafungwa waliokamatwa na dawa hizo hivyo inafanyika utaratibu wa
kuwasafirisha.
Mintanga alikuwa akikabiliwa na mashitaka ya kula njama na kusafirisha
dawa za kulevya zenye uzito wa Kilo 4.8, kutoka Tanzania kwenda Mauritius kwa
kuwatumia wachezaji wa timu ya Taifa ya Ngumi za Ridhaa pamoja na watu
waliosafiri katika msafara huo ambao walidaiwa kuwa ni mashabiki.
Jaji huyo alisema kwa mujibu wa ushahidi ushahidi uliotolewa ni dhaifu
hakuna ushahidi unaoonesha Mintanga alikula njama na alisafirisha dawa za
kulevya kama mashitaka yanavyoeleza.
Jaji huyo anaungana na hoja ya wakili wa mshitakiwa, Jerome Msemwa
hakuna ushahidi dawa zilizokamatwa kuletwa mahakamani au picha za dawa hizo.
Utata wa uzito wa dawa hizo pia ushahidi wa upande wa mashitaka
ulikadiria uzito na thamani za dawa hizo kwa kupiga simu bila kuziona.
Aidha ni ngumu kwasababu dawa hizo
zilikamatwa nchini Mauritius hakuna ushahidi wa dawa hizo na kesi hiyo ambayo
inamkabili mshitakiwa Mintanga, ushahidi wa Charles Ulaya ambaye ni mpelelezi
wa shauri alidai uzito wa dawa hizo ulikuwa Kg 4.8 na ushahidi mwingine
unaonesha ni Kg 6.
|
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...