Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London, Bwana Yusuf Kashangwa, akihutubia kwenye Semina kuhusu Utalii, Tanzania. Semina ambayo ilifanyika siku ya Jumamosi Tarehe 13 October 2012 katika mji wa Redditch, nchini Uingereza. Semina ambayo ilihudhuriwa na Wataalam na Wawakilishi mbalimbali kutoka katika sekta ya Utalii, iliyoandaliwa na Britain Tanzania Society kwa kushirikiana na Redditch One World Link (ROWL), Uingereza.
Mkurugenzi, Bwana Yusuf Kashangwa, akimkabidhi Mstahiki Meya wa Mji wa Redditch, Bwana Allan Mason, zawadi kutoka Tanzania, kama heshima na kuthamini mchango wa Ushirikiano mwema kati ya Mji wake wa Redditch na Tanzania. Mstahiki Meya, Allan ameahidi kuetembelea Tanzania Mwakani.
Baadhi ya Wawakilishi katika Semina hiyo pichani, wakisikiliza kwa makini Mada mbalimbali zikitolewa kuhusu Utalii, Tanzania
Wawakilishi kutoka sekta mbalimbali ya Utalii, waligawanywa kwenye makundi, kujadili changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika kusaidia kukuza na kuboresha Utalii Tanzania
Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara, London, Bwana Yusuf Kashangwa (kwanza kushoto), akiwa kwenye Picha ya pamoja na Mstahiki Meya wa Mji wa Redditch, Bwana Allan Mason, mara baada ya kumalizika kwa Semina hiyo. Wa kwanza kulia, Bwana Mohamed, afisa kwenye Kituo cha Biashara, London.
=======================
Hayo yalikuwa ni maoni ya wataalamu mbalimbali wa masuala ya
utalii, mazingira na maendeleo waliyoyatoa kwenye semina iliyoandaliwa mjini
Redditch kujadili Hali ya utalii nchini Tanzania. Semina hii iliandaliwa kwa
ushirikiano wa Redditch One World Link (ROWL)
na Britain-Tanzania Society (BTS), ilifanyika
siku ya Jumamosi Terehe 13 October 2012, na mada kadhaa ziliwasilishwa na
kujadiliwa na wana semina wapatao 150 hivi. Mgeni rasmi katika semina hiyo
alikuwa ni Mstahiki Meya wa Mji wa Redditch, Bwana Allan Mason.
Mji wa Redditch kupitia Shirika lisilo la kiserikali la
Redditch One World Link (ROWL) una uhusiano wa kirafiki na mji wa Mtwara nchini
Tanzania tangu mwaka 1985.
Baada ya hotuba ya makaribisho ya mgeni rasmi, Mkurugenzi wa
Kituo cha Biashara cha Tanzania Ubalozini London, alikuwa wa kwanza kuwaeleza
wana semina juu ya vivutio mbalimbali vilivyoko nchini Tanzania na pia juu ya
sera ya Utalii endelevu inayotekelezwa na serikali ya Tanzania. Aligusia vipengele
muhimu vya sera hiyo kuwa ni kuongeza mchango wake katika pato la Taifa, kujali
maslahi ya Taifa , ya watu wake, kuhifadhi mazingira na rasilimali nyinginezo
kupitia mikakati na mipango mbalimbali na
kusimamia utekelezaji wake na kwa kuwashirikisha wadau wote bila ya kusahau wananchi wa kawaida
kokote waliko katika maeneo yenye vivutio asilia vya kitalii .
Watoa mada wengine walikuwa ni Bw. Nigel Nicoll, Mkurugenzi
Mkuu wa African Travel and TourismAssociation (ATTA)
aliyeongelea juu ya changamoto wanazokumbana nazo wadau wa utalii, Mark Watson,
Mtendaji Mkuu wa Tourism Concern aliyeongelea
juu ya utalii, mazingira na kujali maadili. Bi Catherine Brenan alielezea
uzoefu alioupata baada ya kupanda mlima
Kilimanjaro, akichangisha fedha za kumalizia jengo la shule.
Kama ilivyo BTS, ROWL hujihusisha na kukuza mahusiano ya kirafiki, kubadilishana uzoefu na kusaidia nyanja mbalimbali za maendeleo,
kijamii , kiuchumi na kiutamaduni.







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...