Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili katika uwanja wa ndege mjini Quebec, Canada tayari kwa kuhudhuria mkutano wa 127 wa chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaotarajia kufunguliwa rasmi kesho tarehe 21 Oktoba, 2012 na kumalizika 26 Oktoba . Makinda ameongoja ujumbe wa wabunge wanne kutoka Tanzania, ambapo zaidi ya maspika wa nchi 150 duniani wakiongoza ujumbe wa wabunge kutoka Nchi zao watashiriki mkutano huo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiteta jambo kuhusu maandalizi ya awali ya mkutano na afisa kutoka Bunge la Canada mara alipopokelewa baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege mjini Canada kuhudhuria mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani. Kulia ni Mhe. David Kafulila na Mhe. Hamad Rashid waliongozana na Mhe. Spika katika Mkutano huo nchini Canada.
Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Canada Joseph Sokoine akimkabidhi Mhe. Spika taarifa ya maandalizi ya mkutano huo pamoja na hali ya kisiasa ilivyo nchini Canada baada ya kuwasili kuhudhuria Mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU).Picha na Owen Mwandumbya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hamadi rashidi anaendelea kuula kama kawaida mikwara ya cuf kwishinei

    ReplyDelete
  2. Huyu mzungu anawakagua kabisa Msije kuzamia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...