25 SERENGETI BOYS WAINGIA KAMBINI
Kikosi
cha wachezaji 25 wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka
17 (Serengeti Boys) kimeingia kambini leo (Oktoba 21 mwaka huu) jijini
Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya raundi ya mwisho ya michuano ya
Afrika kwa vijana.
Serengeti
Boys ambayo iko chini ya Kocha Jakob Michelsen itacheza mechi hiyo ya
raundi ya tatu na mshindi kati ya Congo Brazzaville na Zimbabwe ambapo
tayari Congo Brazzaville imefanikiwa kupata ushindi wa ugenini wa mabao
2-1. Mechi ya marudiano itachezwa jijini Brazzaville kati ya Oktoba
26-28 mwaka huu.
Katika
mechi hiyo ya raundi ya tatu, Serengeti Boys itaanzia nyumbani katika
mchezo utakaofanyika Novemba 17 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, wakati
mechi ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liko katika mikakati ya kuhakikisha
Serengeti Boys inapata mechi mbili za kirafiki za kimataifa kabla ya
kumvaa mshindi kati ya Congo Brazzaville na Zimbabwe. Fainali za Afrika
kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitafanyika Machi mwakani nchini
Morocco.
KAMATI YA LIGI YAIONYA AFRICAN LYON
Kamati
ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeipa onyo kali
timu ya African Lyon kutokana na washabiki wake kuweka bango
lililoandikwa ‘We believe in 0777’ kwenye mechi yake dhidi ya Azam
iliyochezwa Oktoba 6 mwaka huu Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Bango
hilo ambalo si la mdhamini wa Ligi Kuu ya Vodacom halitakiwi kuonekana
tena kwenye mechi ambazo African Lyon inacheza vinginevyo Kamati ya Ligi
itachukua hatua kali dhidi ya timu hiyo.
Kamati
ya Ligi imezikumbusha timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom
kuzingatia kanuni zinazotawala ligi hiyo ili iweze kuendeshwa kwa
ufanisi.
PAMBANO LA YANGA, RUVU SHOOTING LAINGIZA MIL 47/-
Pambano
la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Ruvu Shooting lililochezwa jana
(Oktoba 20 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa
wenyeji Yanga kushinda mabao 3-2 limeingiza sh. 47,615,000.
Watazamaji
8,233 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio
vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000, na sh. 20,000 huku kila klabu
ikipata mgawo wa sh. 8,420,578.47 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 7,263,305.08.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 120,000,
kamishna wa mechi sh. 203,000, waamuzi sh. 381,000, mwamuzi wa akiba sh.
70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium
technical support) sh. 2,000,000.
Umeme
sh. 300,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000,
ulinzi wa mechi sh. 3,500,000 wakati tiketi ni sh. 2,959,100. Gharama za
mchezo sh. 2,806,859.49, uwanja sh. 2,806,859.49, Kamati ya Ligi sh.
2,806,859.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
1,684,115.69 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 1,122,743.80.


Million 8.4 za kitanzania ni 3000 british pounds, huu ni mshahara wa wiki wa mchezaji wa daraja la tatu la Uingereza, bongo ndio mgao wa timu nzima ya ligi kuu, duuuh kweli bongo tambarare. Ndio mnataka turudi huko wakati huku nje kuna opportunities for our kids kuliko hiyo nchi ya mafisadi, wanaocheza wanapata pesa ndogo waliokaa ofisini ndio wanakula panga.
ReplyDelete