Hali ya Usafiri wa kutoka Lindi kwenda wilayani Ruangwa imeendelea kuwa
tatizo,hali inayopelekea Mabasi ya Abiria kujaza abiria zaidi ya
ilivyopangwa na Sumatra kama inavyoonekana pichani huku ikimlazimu
kondakta wa basi kukosa nasafi na kulazimika kukaa katika ngazi huku
basi hilo likiendelea na safari...Baadhi ya abiria wameiomba mamlaka
hiyo ya Usafirishaji kuangalia hali hiyo ambayo ni ya hatari sana.
Kondakta wa Basi hili akiwa amening'inia kwenye ngazi huku basi likiendelea kwenda.
Abiria wakiendelea kupanda basi ambato tayari linaonekana limeshajaa.


sumatra hawana mabasi kwamba watayapeleka huko Ruangwa, sumatra sio wanaowalazimishi watu wazima wenye akili zao kupanda mabasi yaliojaa kupita kiasi, iombe serikali yako ya "maisha bora kwa kila mtanzania" itandike lami hiyo njia uone jinsi mabasi yatakavyoongezeka!!
ReplyDelete