habari Kaka Michuzi 

Mimi ni kijana ninaye ishi nje ya nchi na huwa nina kawaida ya kuwatumia ndugu zangu zawadi mara kwa mara ila shirika la posta Tanzania kitu wanachokifanya si cha kiungwana. 

Kwani wiki iliyopita nilituma kifurushi Tanzania na nikakilipia kila kitu sasa jana mdogo wangu ameenda kuchukua pale posta mpya wamemwambia atoe shilinga Elfu themanini (80000) au atoe rushwa ya shilingi elfu thelathini (30000) ili wampe mzigo.

Na kilichopo ndani hakina thamani ya hela hizo wanazozitaka, je hii ni haki na hii sio mara ya kwanza naona sasa imefika kikomo, kwani nikituma kwa Dhl hakuna kitu kama hicho. nakwandikia ili ujumbe ufike kwa wahusika wanaofanya shughuli hii. 

Aariq - Toronto

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. sasa na wewe si uache kutumia posta?? Kwanini hutumii DHL ambayo haina matatizo?? Shida zingine tunajitakia wenyewe.

    ReplyDelete
  2. All these are not maters of life and death. But jamaa hawa wizi wanakera sana.Kwa nini idara inayohusika na polisi hawachukui hatua kukomesha cancer hii.They have to put fear of God in these kupes.

    ReplyDelete
  3. kaka hilo ni lazima,mie ndugu zangu walishaniambia hawana haja na parcel tena maana gharama za kulipia ni nyingi mnooo,unatuma pair ya raba na perfume unalipia elfu 80000 ya nini??ni heri utume hela wanunue huko home..pole sana na posta angalieni hii sio nzuri,

    ReplyDelete
  4. Mimi nina harisa kama zako ndio maana nilichukia sasa niliposoma hapa kwamba shirika la posta la tanzania limepata tuzo ya kimataifa kwa huduma bora!!!!

    ReplyDelete
  5. Ndiyo maana shirika linakufa! Waziri husika inabidi afwatilie hili swala maana ni mchezo wa muda mrefu sana.
    Halafu pia wanatabia ya kuiba vitu wanakwambia parcel haijafika wakati inaonyesha imefika.

    ReplyDelete
  6. ukisikia ufisadi ndo huu watu wana tamaa ya kutajirika haraka haraka katika nchi hii hawajui chochote zaidi ya hilo wako tayari kufanya lolote,inasikitisha kweli kweli ningekuwa niko bongo ningekusaidia wangu kwa sababu wote pale posta nawajua na kifurushi ungekipata bila ya rushwa yeyote ile lakin ndo hivyo niko majuu kimasoma.

    cha kufanya tuma barua kwa raisi na mtendaji mkuu wa post okay nakuahidi mdogo wako atapata mzigo wake okay

    pole sana wangu ndo maisha ya kibongo bongo rushwa nje nje asikudanganye mtu kwamba wanafuata sheria no way out or in rushwa kwenda mbele nawajua sawa ndugu zangu pale posta lakin kwangu wanakiona cha moto

    ReplyDelete
  7. USIPATE TABU TUMA MZIGO WA RWANDA NA HULIKPI CHOCHOTE NA HATUPOTEI KUNA WAKALA KIBAO HUKU HALAFU WAO WANAUSAFIRISHA MPAKA TANZANIA KWA MAGARI BURE BURESHI
    ACHANA NA POSTA TANZANIA WEZI WAKUBWA HAO

    ReplyDelete
  8. jamani kuna kitu sijaelewa, kwa kawaida mzigo wowote utokao nje ya nchi hata kama ni zawadi ni lazima ulipiwe ushuru na kodi mbalimbali kwa mujibu wa taratibu za nchi kupitia TRA kulingana na thamani ya mzigo husika haijalishi ni njia gani ya usafiri inatumika kuusafirisha, sasa kama mtu kaombwa rushwa hiyo ni kitu kingine pia kama amelipishwa kinyume na thamani husika pia ana haki ya kuwasiliana na wahusika kutatua tatizo husika

    ReplyDelete
  9. Naona suluhisho hapa kwenye biashara hulia ni kuacha kutumia shirika la posta Tanzania na kutumia mashirika mengine yanayo deliver kama DHL nk. hata hizo njia za Rwanda watu wameanza gundua kwasababu ya posta. Mimi nilituma ubuyu kiasi kwa mdogo wangu Doha,ukaishia njiani,sijui jamaa wameamua kula kama lunch?mambo ya aibu hata shemeji wangu ambae sio mtanzania kashangaa.Mimi situmii posta tena. Kweli cheap is expensive

    ReplyDelete
  10. mdau wa kwanza ndugu yangu pole pole si wote wenye uwezo wa kutuma DHL unafikiri ingekuwa rahisi kutuma kwa njia hiyo si angetuma kuwa muugwana wa kuelewa ndugu yangu situation za binadamu siyo kupayupa payuka na hao wanaotaka rushwa kweli wanavyofanya si vizuri lakin mtu ana familia na wazazi wanamtegemea na mshahara haumtoshi na aanakuja bi shororo anataka mzigo wake kutoka majua si anajua pesa wanazo ndo maana ana dai rushwa

    siyo kama nawatetea lakin vikiriyeni maisha ya wenzenu na kwa nini kila leo watu wanataka kuwa wanasiasa, wabunge, mawaziri etc kama hakuna raha ya dunia pesa nje nje danganya raia wewe unatia pesa nje nje

    kuweni wakutafakari kwa nini mtu anafanya hivi na vile siyo kila leo kubwabwaja katika blog ya misupu michuzi

    ReplyDelete
  11. Mdau wa kwanza nadhani hajaelewa ni kwa nini huyu bwana ameamua kuweka hadharani udhaifu huu wa shirika la posta lengo ni kwamba wasomapo hizi habari basi wajirekebishe au wahusika kwa upande wa wizara waonapo hizi taarifa waweze kufuatilia pia hata kwa wasomaji ambao pengine hawafahamu unyama huu wa posta kupitia uzoefu wake waweze fahamu sasa unapomwambia si atumie D.H.L kwa maneno mengine ni kwamba unamziba mdomo ili unyama huu usijurikane na pia kumbuka D.H.L ni shirika la nje hivyo unapalilia kulikosesha taifa fedha kirahisi namna hiyo.
    Acha hasira na maamuzi ya haraka.

    ReplyDelete
  12. Duh hii ya kutuma parcel through Rwanda ni kali sana na changamoto kwa wadau wanaohusika na vipeto pale Posta, ikiwa ni Posta wenyewe na wwatoza ushuru TRA. Ni vema waathirika wakatoa taarifa kamili ili hatua sahihi siwezi kuchukuliwa.

    ReplyDelete
  13. Dawa yao hawa tuma ANTHRAX (KIMETA) harafu ndugu zako wasiende kuchukua. WAKIFUNGUA TU- WAMEKWISHA Hahahahaahhaaaa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...