Kampuni ya simu za mkononi Vodacom, ambao pia ni wadhamini wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, wamefikia muafaka na klabu ya Yanga juu ya kutotumia jezi zenye nembo nyekundu.
Vodacom imefikia hatua hiyo kufuatia Yanga kupeleka maombi yao ya kuomba kutotumia nembo hiyo nyekundu katika jezi zao.
Kufuatia maombi ya klabu ya Yanga kupitia kwa viongozi wake na baraza la wazee, vodacom imeona ni busara kuwasikiliza Yanga maombi yao na hivyo kuamua kuipa nafasi ya kuchagua nembo moja kati ya tatu.
Vodacom imetoa aina tatu za nembo na Yanga inapaswa kuchagua moja kati ya hizi nembo tatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. kati ya hizo nembo tatu hiyo ya mwisho (white & black) ingeondolewa kabisa na badala yake ikawekwa Kijana na njano,kwahiyo ya kwanza Njano na nyeusi,ya pili kijani na nyeusi na ya mwisho ikawa kijani na njano ambayo nahisi itakuwa best kwa Yanga.huu ni mtazamo wangu,na nitaheshimu na wenzangu kama watachangia mawazo yao.

    ReplyDelete
  2. Mdau wa MaguOctober 19, 2012

    Grrrrrrrrrrrrr Wewe MagangaONe kwanza vua hilo koti lako jekundu.
    Halafu rudia nikusikie ulitaka kusema nini, hauelweki na hautaeleweka kamwe. na hiyo nembo nyeupe (namba tatu) hatuitaki pia, wanaitumia wale jamaaa. Rangi zilizobaki zozote poa.Nipo alergic na hizo rangi Grrrrrrrrrrr

    ReplyDelete
  3. Nembo ya kijani ikiwa itazungukwa na rangi ya njano na nembo ya njano ikiwa itazungukwa na rangi ya kijani. Nyeupe haina nafasi.

    ReplyDelete
  4. Nawauliza Vodacom, kila timu ikitaka rangi yake itakuwaje? Huu ni uswahili!!!

    ReplyDelete
  5. Kutumia nembo yoyote kati ya hizo tatu ni upotoshaji. Rangi za Yanga ni Kijani na Njano kwa zote mbili kuwepo pamoja.

    ReplyDelete
  6. Sasa kaka michu mbona zote zina rangi nyeupe au nayo ni rangi ya yanga

    ReplyDelete
  7. Zote hazifai,hatudanganyiki!!!!

    ReplyDelete
  8. Unaweza kudhani ni nembo zinazocheza uwanjani.

    ReplyDelete
  9. Nadhani nembo zote si sahihi kwani ni vyema Vodacom ikabaki kama ilivyo na yanga halikadhalika.

    ReplyDelete
  10. CHUKUA HIYO YA KIJANI, LAKINI HAPO PENYE NYEUPE UWEKE NJANO. KWISH, ITAKUWA NA KIJANI, NJANO NA NYEUSI, ANGALAU KIDOGOM. BUT KUCHAGUA KAMA ULIVYOULIZA, NO ZOTE HAZIFAI. HEBU TUONE MDAU YUPI ATASHINDA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...