Kibaka alieanaswa akiiba vitu kwenye mkoba wa mama (huyo mwenye kilemba) akiwa amewekwa chini na wasamalia waliomnasa kabla ya kuanza kumtembezea kichapo alipobaini kuwa kuna vitu vingine alivyokuwa ameviiba awali.kibaka huyu amenaswa mchana wa leo katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Kichapo cha nguzu kikaanza,jamaa analia kama mtoto mdogo huku akisema sirudiii tena jamaniiii....
hapa ni bakora kwa kwenda mbele.
Baadae akasamehewa na kuamria kuondoka eneo hilo.
Msamalia mwingine alijitokeza na kumsukuma ili aondoke na asionekane tena katika eneo hilo.
Kibaka yuleeeeeee......








tuna safari ndefu sana katika upande huu ......
ReplyDeleteHii ni mbaya sana,kumlimba binadamu mwenzio siyo uugwana!
ReplyDeleteMpelekeni polisi badala ya kumpiga au mtafutieni ajira aache kuiba. Njaa tu inamsumbua.
ReplyDeleteutawala wa sheria binafsi.
ReplyDeletenjaa haziwezi kuisha ikiwa walalahoi wanashindwa kumiliki kitu mlo
ReplyDeletena kwa upande wa mafisadi wanashindana kwa kutaka kumiliki ndege maana magari na majumba sasa sio kitu kwa mafisadi.
mpeni kula mfa njaa mwenzetu huyo msimuongezee shida ya kutafuta madawa kwa kumtia majeraha
Huu ulikuwa ni mkutano uliohudhuriwa na wakubwa wa nchi lakini sheria imevunjwa, watu wamechukua sheria mkononi badala kumpleka polisi.
ReplyDeleteWAZO JIPYA:
ReplyDelete'''NJAA HAINA UBAUNSA''''
Nafikiri tujaribu kufungua ukurasa mpya wa maisha na sasa badala ya kuwapiga vibaka na wezi tuwakamate na kuwauliza wanaiba kwa nini?
Wakijibu nadhani Majibu yao hayatakuwa nje ya hapa:
1.Nina njaa sijakula.
2.Nina majukumu nategemewa.
3.Ninaumwa natafuta hela ya matibabu.
4.Akili yangu sio timamu nina ugonjwa wa akili lakini pana wakati napata nafuu najitambua.
Sasa wandugu kwa majibu mojawapo ya hayo manne (4) hapo juu, nadhani upo uwezekano wa mbadala kuliko kuwapiga!
TUTAFANYA HIVI KWA MAJIBU YA MASWALI HAYO MANNE HAPO JUU:
1.Jumuia hasa za Kiimani Misikiti na Makanisa watoe huduma za msaada wa chakula cha bure angalau mlo mmoja kwa siku.
2.Wapewe kazi za Kijamii ili wapewe angalau chochote kujikimu.
3.Wapewe Msaada wa Matibabu ya bure vituo vya Afya.
4.Wapelekwe vituo vya Matibabu ya Afya ya akili.
HII IWE KWA WEZI WAKIKAMATWA.