Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
akifurahia jambo na Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Bw Salum Mwalim mara
baada ya kupokea hundi yenye thamani ya shilingi Milioni Kumi na Tano mchango
wa Vodacom Foundation kwenye mfuko wa maendeleo ya watu wenye ulemavu Zanzibar.
Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa Vodacom Bi
Joseline Kamuhanda. Vodacom ilikabidhi hundi hiyo katika hafla ya uzinduzi wa
mfuko huo iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mjini Zanzibar.
Mkuu
wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi Joseline
Kamuhanda.akitoa salaam za Vodacom Tanzania wakati wa hafla ya chakula cha
usiku iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar kuchangia
mfuko mpya wa maendeleo ya watu wenye ulemavu Zanzibar
iliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Zanzibar. Vodacom Tanzania ilichangia
Shilingi Milioni Kumi na Tano kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii - Vodacom
Foundation.
Wafanyakazi
wa Vodacom Tanzania kutoka kushoto Meneja Mahusiano ya Nje Bw. Salum Mwalim,
Mkuu wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano Bi. Joseline Kamuhanda na Meneja
Kanda ya Zanzibar Bw. Mohamed Mansour wakipokea utambulisho wa kuwa miongoni
mwa wadhamini wakuu waanzilishi wa mfuko wa Manedeleo ya watu wenye
ulemavu Zanzibar wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfuko huo iliyofanyika
mwishoni mwa wiki Zanzibar. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Habari,
Utamaduni, Utalii na Michezo wa Zanzibar Mh. Said Ali Mbarouk.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
akihutubia wadau mbalimbali waliohudhuria hafla ya chakula cha jioni
iliyolenga kuuzindua rasmi mfuko wa maendeleo ya watu wenye ulemavu
Zanzibar mwishoni mwa wiki mjini Zanzibar. Wa kwanza kushoto ni Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad. Hafla hiyo iliandaliwa na
Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Vodacom Tanzania ilichangia
Shilingi Milioni Kumi na Tano kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii - Vodacom
Foundation.
Kwa habari kamili BOFYA HAPA
Kwa habari kamili BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...