Kwako Mkuu wa Polisi kanda maalum, Dar es salaam
Sisi ni mkaazi wa Kipunguni A Ukonga Banana, jijini Dar es salaam.
Katka wiki za hivi karibuni kumekuwa na matukio ya unyang'anyi wa kutumia silaha na wizi wa mifugo katika eneo letu hili la Kipunguni . Tumeripoti matukio mengi haya katka kituo cha Stakishari Ukonga lakini mpaka leo hakuna hatua ya msingi iliyochukuliwa.
Usiku wa kuamkia leo kumetokea tukio lingine la ambalo majambazi/wezi wamemchoma kwa kisu tumboni kijana mmoja aitwae Peter na amelazwa hospital hivi sasa lkn pamoja na hayo police hawajafika ktk eneo la tukio na tunashindwa kuelewa wajibu wa jeshio la police ktk kulinda raia wake. Je kodi zetu zinatumika kuwalipa mishahara ya bure bila wajibu?
Je, raia tuanze kuchukua hatua mikononi?
Tunaomba majibu ya haraka na msingi
hili kwa kuwa hali hii sasa haivumiliki tena
Wako Wakaazi Kipunguni
Kaka poleni sana lakina napenda kukumbusha kwamba Polisi hawawezi kazi hiyo,kazi wanayoiweza wao na kuifanya kwa ukamilifu mkubwa ni Kuwapiga Wiaslam wanapoandamana au wafusi wa vyama vya upinzani tu.Nje ya kazi hii hawana kazi yoyote wanayoiweza sanasana watachukua rushwa tu.
ReplyDeleteMkuu wa Police hili jambo chukulia MUHIMU sana hawa watu wako wa kituo cha Stakishari ni kero wanaaibisha jeshi la polisi kwa kweli fanyia kazi haraka wakiambiwa ukweli unatishiwa au unakamatwa pasipo kuwa na kosa. Wanaaibisha sana sana kumeoza Stakishari, na pia wao wanapenda kusikilizwa na kuhukumu mtu utadhani ukikamatwa tayari wanathibitisha kosa hivyo kufanya kazi ya makahama kwa raia wasio jua sheria si vizuri, Watanzania wengi unajua si watu wa mifarakano hivyo akifanya kosa japo si kwa kusudia likifika polisi tu ujue umekwisha kisa Watanzania hatujui sheria nyingi Stakishari bila pesa hupati dhamana. kama kuna kesi za mifarakano ya hapa na pale usuluhushu umewaomba polisi lazima wale pesa yako, sasa wanadhani tutawapenda kweli? Wamezidi kuonea sana raia ukizingatia hali ya maisha ni ngumu sana. nchi za wenzetu rushwa ipo lakini huwezi kugundua hata kidogo inatumika ipasavyo lkn kweli too much hata dhamana nayo utoe pesa??????!!!!!!!!!!
ReplyDelete