SHUURA YA MAIMAMU MJINI BAGAMOYO: Inapenda kuwatangazia waislamu wote wa miji ya jirani na Bagamoyo na kwengine kote nchini kuwa, Waisilamu wa Bagamoyo kwa ujumla wao wataungana na wenzao kote duniani katika kusherehekea sikukuu hii. Ili kufanikisha furaha hii, waislamu wameweka nia ya kwenda na familia zao kwenye ufukwe wa bahari kama ilivyo katika sikukuu zingine.
Nia na madhumuni ya kuandaa utaratibu wa kwenda kushereherekea kwenye fukwe, kwanza ni kuwapa fursa waisilamu wa Bagamoyo kuweza kufurahia pamoja na family zao.
Pili kama inavyofahamika siku za sikuku fukwe za Bagamoyo zimekuwa zikitumika kwa mambo machafu yakiwemo ngono, ulevi, uvutaji bangi, ujambazi, na mengi mengineo yasiyopendeza katika jamii kiasi cha kuvuruga amani, heshima na uvunjikaji wa maadili.
Machafu ambayo yamekuwa yakifanywa na vijana wanaotoka nje ya mji wa Bagamoyo baada Serikali kuwapiga marufuku katika fukwe za Ndege Beach na Coco Beach na maeneo mengineyo. Kutokana na machafu haya, waislamu na wote wenye maadili mazuri wamakuwa wanazuilika kutumia fursa hii aliyotoa Allah Subhana Wa Taalah bure.
Hivyo dhumuni la pili nikutumia fursa hii kuelimisha jamii kwa vitendo njia sahihi ya jinsi sikukuu za Kiisilamu zinavyopaswa kusherehekewa. Elimu ambayo itasaidia kupunguza maasi na machafu ambayo yamekuwa yakihusishwa na sikukuu za Kiisilamu.
Dhumuni ambalo bila shaka linaungana na juhudi za Serikali za kuondosha mambo machafu kama utumiaji wa madawa ya kulevya, kufanya ngono sehemu za wazi, ubakaji, na uporaji, mambo ambayo hutendeka kwenye fukwe na kiujumla hayafai katika jamii.
Katika sikukuu hii , kumeandaliwa michezo mbali mbali ikiwemo mbio za pikipiki, baiskeli, sarakasi, mashindano ya ngalawa, mpira wa miguu.
Michezo hii itafanyika katika eneo kati ya Chuo cha Sanaa na iliyokuwa Hotel ya BADECO.
Maeneo mengine ya Msalabani na Ufukwe wa Hunters yatakuwa wazi kwa watumiaji wengine
WAISLAMU WOTE MNAKARIBISHWA


Nina penda kujiunga mkono na Wasilamu wa Bagamoyo kwa sharehe ya sikuku ya Eid watao andah. Huwezi kulala mika bila konesha mfano na ku elimisha familia na jamii. Eid Mubarka kwa wote.
ReplyDeleteHongereni sana kwa uamuzi huo muliochukuwa wa maana sana.
ReplyDeleteMwenyezi Mungu awajaalie iwe Idi ya kheri na fanaka musherekee kwa amani bila ya matatizo.