Jumapili 14 Oktoba , 2012 watanzania mjini
Roma walipata nafasi ya kuungana na watanzania wengine wote, katika
kuadhimisha siku ya Baba wa Taifa, Mwalimu J.K. Nyerere. Maadhimisho
hayo yalifanyika katika Chuo Cha Kipapa cha Mt. Petro, mjini Roma,
kwa Ibada ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Mhashamu Askofu Mkuu
Protas Rugambwa, akishirikiana na Mwadhama Kardinali Pengo, Askofu
Mkuu Lebulu wa Jimbo kuu la Arusha pamoja na Askofu Libena wa jimbo
la Ifakara.
Kwa habari na picha zaidi tembeleeni
www.watanzania-roma.blogspot. com
Mwadhama Kardinali Pengo
Mh. Dr. Balozi Msekela akiwa kwenye meza kuu na Viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi Wakatoriki Roma pamoja na Mhashamu Askofu Mkuu Protas Rugambwa na Askofu Mkuu Lebulu wa Jimbo kuu la Arusha.
Watanzania wengi wakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mh. Dr. James Alex Msekela, walishiriki ibada
hiyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Roma akibadilishana mawili matatu na padri


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...