Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika picha ya pamoja na Mwenyeji wake Mhe. Laurent Fabius, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa ofisini kwake jijini Paris leo.
Mheshimiwa Waziri Bernard K. Membe (Mb.) , Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika mazungumzo na Mhe. Abdou Diouf, Katibu Mkuu wa La Franchophonie na Rais Mstaafu wa Senegal alipofanya nae mazungumzo ofisini kwake Paris leo. Wa kwanza kushoto ni Mhe. Begum Karim Taj, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa.
Mhe. Waziri Membe na mwenyeji wake Mhe. Abdou Diouf katika picha ya pamoja na ujumbe wao mara baada ya mazungumzo. 

Mhe. Waziri Membe yuko nchini Ufaransa kuwasilisha ujumbe maalum wa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa Ulinzi na Usalama kwa Mhe. Francois Hollande, Rais wa Ufaransa. Mhe. Waziri Membe amewasili leo asubuhi na kufanya mazungumzo na Mwenyeji wake Mhe. Laurent Fabius, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa ofisini kwake jijini Paris. 

Mhe. Membe aliwasilisha ujumbe wa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama kwa Mhe. Francois Hollande, Rais wa Ufaransa. Tanzania ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, chombo kinachoshughulikia migogoro na usuluhishi katika ukanda wa SADC.

 Baadaye, Mhe. Waziri Membe alifanya mazungumzo na Mhe. Abdou Diouf, Katibu Mkuu wa La Francophonie na Rais Mstaafu wa Senegal. Mhe. Waziri Membe anatarajia kumaliza ziara yake kesho kwa kukutana na Mshauri wa Rais Hollande wa Masuala ya Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...