Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kusisitiza utaratibu wa usajili wa magari ya Umma unafuatwa na kutafanyika zoezi rasmi la kurejesha usajili wa magari yote.Serikali imetoa muda wa hadi kufikia Novemba 15,2012 magari ya Umma yaliyo na namba za kiraia, yarejeshwe namba stahiki za magari ya Umma . Baada ya hapo Operesheni hiyo itakamata magari, pikipiki, bajaj na mitambo ya umma,Vilevle kutakuwa na aina ya namba za usajili zitakazotumika kama ST, PT, MT,JW, DFP, CW, SM na ,SU.Hadi sasa serikali imesajili vyombo vya moto,123,431 yakiwemo magari,,pikipiki,bajaj na mitambo ya umma.Kulia ni Mkuu wa Polisi kikosi cha Usalama barabarani,Kamanda Mohamed Mpinga
Kaibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Hebert Mrango (ailesimama)akifafanua jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
"kuna walionununua magari ya serikali lakini bado hawajayabadilisha namba za usajili" ndivyo anavyoonekana kukumbusha kamanda Mpinga kwa Waziri Magufuli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mtakamata na ya Ikulu na Ofisi ya makamu wa Rais???

    ReplyDelete
  2. Kibao kipya hicho ngoja nikinunue kabla hakijachuja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...