Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki
Jimbo la Bukoba, Method  Kilaini

Kwa masikitiko makubwa nimesoma katika gazeti la Mwananchi kwamba nimeiponda safu ya uongozi na sekretariati ya CCM. 

Mimi sijaongea na gazeti lolote juu ya uongozi wa CCM na wala sina nia au sababu ya kuuponda uongozi huo. Ni vibaya kwa gazeti lo lote lile kutumia jina la mtu kwa kueneza maoni yake. 

Kama ni waugwana natumaini watasahihisha waliyoyaandika. Nasikitika sana kwa waliokwazwa na hilo. 

Askofu Method Kilaini
Bukoba Catholic Diocese

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Askofu Kilaini,kwanza nikusalimie-"Kristu"..Gazeti la Mwananchi ni kati ya magazeti Makini na linaloheshimika Tanzania,na limekunukuu.Kama haujaongea nalo basi litakuwa la kiungwana na kukanusha.Ili kuepukana na adha hizi ni bora kuacha kabisa(na viongozi wengine wa dini) kujiusisha kabisa na masuala ya siasa na hasa hizi siasa zetu za Tanzania.

    David V

    ReplyDelete
  2. Pole sana Baba Askofu. Kwa kweli nimeshangazwa sana na Gazeti kama Mwananchi kuandika habari ya uongo! Ni gazeti ambalo siku zote ninadhani kuwa li miongoni mwa magazeti yenye kufuata misingi na weledi wa taaluma ya uandishi habari, kumbe sivyo. Hii ni aibu jamani. Mnatuharibia taaluma. Tuamini gazeti lipi sasa?

    ReplyDelete
  3. Mwananchi ni gazeti makini lakini mara kadhaa gazeti hili huandika habari za kugombanisha, yaelekea huwa kunamtu anajitokeza kuwanunua baazi ya waandishi kwa lengo la kuchafua majina ama taasisi fulani. MWANANCHI KUWENI MAKINI.

    ReplyDelete
  4. Mwananchi siyo Gazeti makini mala nyingi limekuwa bias na negative kwa serikali,katika kila toleo lake la kila siku ile habari mbaya ya uzushi ndiyo hupewa kipaumbele.pole sana Baba askofu hii siyo dalili njema kwa Kanisa na siasa za Tanzania

    ReplyDelete
  5. David V jifunze uhusiano kati ya siasa na dini kabla ya kushauri viongozi wa dini kujihusisha na siasa. Siasa inajenga bora inajenga maisha bora ya kiimani na siasa mbaya inapoteza maisha ya mtu kiimani hasa hali ya uchumi. Viongozi wa dini wana naafasi kisiasa. Na kwakuwa amesema hakusema lazima aheshimiwe. Kunukuu sio justification ya kusema.

    ReplyDelete
  6. David V. kumbuka viongozi wa dini na waumini wao ni wazalendo vile vile, kuwaambia viongozi wao wasijiushe kisiasa ni kuwanyima haki yao. Mamuuzi yafanywao kisiasa yanawagusa kila mtu.Viongozi wa dini wanaweza kutoa maoni au hapana kwenye msimamo wa hoja mbali mbali na waumini wao wenyewe wanaweza kufikiri kuchukua hayo mawazo au hapana. Hapa kosa kubwa ni kwamba, je mwandishi wa habari alimnukuu askofu akisema hivyo au lah! Na kama si hivyo basi tutalichulia Mwananchi kama gazeti la udaku.

    ReplyDelete
  7. If Tanzania is a secular state then the doctrine of 'separation of religion and the state' should apply, lakini hapa kwetu tumeona mara kwa mara viongozi wa dini wakiingilia maamuzi ya serikali na husuna kanisa katoliki, mara kutoa miongozo na matamko, matokeo yake ndio haya. Gazeti la Mwananchi limekuwa likishabikia mwenendo huo bila ya kukemewa kwa hivyo safari hii wametoa utangulizi wa kile walichokuwa wanakitegemea kufuatia uzoefu wao. Pole sana baba Askofu hili liwe fundisho.

    ReplyDelete
  8. Hivyo wenzenu waliforetell kile walichofikiria Kanisa lingelisema na kukubali this time wamekuwa AMAGEDON. HILI GAZETI NI CHOCHEZI BAINA YA WANANCHI NA SERIKALI, CHADEMA NDIO CHAMA CHAO HIVYO CCM NI KUPONDA MBELE KWA MBELE. SUNGURA ALIKOSA NDIZI AKASEMA MBICHI HIZI HUKU WENZEKE WANAFAIDI. KAMA KUWAELEWA BASI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...