Ni juzi tu kule mjini Dodoma katika shamra shamra za mahafali ya  Chuo Kikuu cha Dodoma aka UDOM, ambapo katika baadhi ya wadau waliokula Nondozzz ni  kijana Dani Hudu. Wazazi ndugu na marafiki wa wasomi pia walishiriki katika shangwe hizo za kula Nondozzzz. Moja ya wazazi hao alikuwapo bondia mkongwe nchini Bw.Iraki Hudu ambaye ndiye baba mzazi wa dogo Daniel  Huddu ambaye kala Nondozzz ya  Geography and environmental studies chuoni hapo. Hongereni sana wasomi wa Udom na wazazi wote 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Daniele Irak Hudu,

    Mtoto wa nyoka ni nyoka, usifikiri kuvaa Makoti ndio 'Ndonga' basi tena?

    Hapo bado, Baada ya Digriii yako ya Ubosi huko UDOM Mzee wako anaweza akakustukiza akakupeleka Chuo cha Boxing!

    ReplyDelete
  2. Irak Hudu,

    Ahhhh Mzee alikuwa na 'mawe' balaa!
    Aliwahi kumchapa ngumi mtu akazimia juu ya Jukwaa!

    ReplyDelete
  3. Irak Hudu,

    Sio mchezo enzi zake alikuwa 'ngumi jiwe' !

    ReplyDelete
  4. Iraq Hudu,

    Mvue Joho lake la Digrii huyo dogo Daniel umwingize kwenye Mazoezi makali ya Boxing!!!

    Lazima Dogo aelewe ya kuwa wewe Mzee wake Mzee Iraq Hudu ni ''JITU KUMBUKA'' katika Tasnia ya Ndondi!

    ReplyDelete
  5. Mzee hudu kamwe Ujuzi hauzeeki!

    Dogo Daniel ili kumpa uhakika wa hatima yake kimaisha ni kuwa na Taaluma Mbadala zaidi ya hiyo Digrii yake ya UDom,

    Inatakiwa siku moja ghafla alfajiri unamstukiza kwa muwamsha na kumwamuru avae Traki na Glovu za mikono halafu umapeleka kwenye Uwanja na kumpigisha kwata la Mazoezi makali kabisa!!!

    ReplyDelete
  6. Hongera sana Iraq Hudu kwa Wasifu wako ktk Ndondi na kumsomesha mwanao Daniel!

    Hongera sana Daniel Iraq Hudu kwa kupata Shahada ya Masomo!!!

    ReplyDelete
  7. Hivi jamani kwa nini tunakuwa na Utamaduni mbaya wa kutokutunza kumbukumbu?

    Ina maana ushiriki wake wote ule ktk timu ya Taifa ya Ndondi Rekodi hakuna?

    Angalieni leo tunamwona Bondia Mstaafu Iraq Hudu kwenye Sherehe za Mahafali ya mwanawe!!!

    Hii ni sawa kweli?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...