·
Eneo la Polisi Oysterbay halijauzwa na haliuzwi.
·
Eneo linalohusika sio
Bwalo la Polisi bali Polisi Oysterbay.
·
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetafuta mwekezaji kwa
lengo la kuwekeza katika eneo la Polisi Oysterbay lenye ukubwa wa ekari 24. Uwekezaji huo utawezesha kujengwa kwa
nyumba za makazi 350 ya Polisi katika maeneo ya Mikocheni na Kunduchi jijini
Dar es Salaam na Kituo cha Polisi cha kisasa katika eneo hilo la Oysterbay.
·
Mshauri Mwelekezi wa Mradi huo ni Bureau for Industrial Cooperation (BICO) ya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam.
·
Mwekezaji aliyepatikana baada ya kufuata taratibu zote za
Manunuzi ya Serikali kufanyika ni Mara Group Ltd. ya nchini Uganda.
·
Tenda ilitangazwa kimataifa.
·
Kampuni 10 zilishiriki katika tenda hiyo.
·
Mkataba wa Awali kati ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na
Mwekezaji huyo umesainiwa tarehe 23 Juni, 2012.
·
Gharama za uwekezaji katika eneo hilo ni karibu shilingi
426.6 bilioni.
·
Kufuatana na Mkataba wa Awali, Mwekezaji huyo atajenga nyumba
za makazi 350 kwa ajili ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam na Kituo kipya
cha kisasa cha Polisi katika eneo hilo, kwa gharama ya shilingi 31.6
bilioni. Fedha hizi zitalipwa kutokana
na tozo atakalokuwa analipa Mwekezaji.
·
Kufuatana na Mkataba wa Awali, Mwekezaji atalipa tozo la
shilingi 4.36 bilioni kila mwaka kama malipo ya matumizi ya ardhi na majengo na
tozo hili litakuwa linapanda kufuatana na mwenendo wa uchumi wa nchi.
·
Kufuatana na Mkataba, ardhi na majengo yote atakayojenga
Mwekezaji yatabaki kuwa ni mali ya Serikali na
yeye atakuwa mpangaji tu.
·
Mwekezaji atajenga Maduka makubwa (Shopping Malls), Hospitali
kubwa ya kisasa, Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya kisasa, Ofisi za kukodisha,
Makazi ya kukodisha na Maeneo ya maegesho ya magari.
·
Mradi utanarajiwa kuanza mwezi Julai, 2013 baada ya kusaini
Mkataba.
·
Mkataba wa Mradi ni wa miaka 50.
(Unaweza pia kutembelea Tovuti ya
Wizara, www.moha.go.tz kupata taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari tarehe 14 Novemba, 2012).
Imeandaliwa
na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Good idea BUT....!!!
ReplyDeleteHii mikataba ya miaka 50, shuti WADANGANYIKA TUWE MACHOOOOO...! Inatakiwa huu uwekezaji uangaliwe kwa jicho l;a 3,4.. Hapo milimani kumewekweza majengo ambayo YANA NYUFA BALAA, hata miaka 50 sidhani kama yatafika. Kama tunataka majengo ambayo mwekezaji anatuachia ni budi kuwe na usimamizi wa kutosha wa kuzingatia QUALITY. Wasiachwe wenyewe,
Yaani POLISI wetu wakakae mbali Kunduchi Mtongani, je wakihitajika maeneo ya Oysterbay, Msasani, Ada Estate, Mwananyamala n.k watafikaje haraka? au Kampuni za ulinzi za binafsi ndiyo watatoa huduma hiyo ya usalama kwa raia?
ReplyDeleteHii kitu inaitwa OPEN GOVT au UWAZI WA SERIKALI, kwa nini hawakushirikisha umma au jamii kabla ya kusaini mkataba wa mradi maana na sisi wadau kupitia POLISI JAMII tungetoa maoni yetu.
Mdau
Maeneo Morocco DSM
ReplyDeleteHii haijakaa vizuri, jeshi la polisi linategemea mwekezaji!!!
Kama hakuna uwezo acheni kwanza, hakuna ulazima wowote wa kutuwekea "Kituo cha polisi cha kisasa" ili iweje? Ki ostabei polisi chetu kiacheni hivyo hivyo maana tunakataa utata.
Mwisho mtapata na sababu za kuleta mwekezaji Lugalo na Mgulani.
Huu uwekezaji sio mzuri kwani muwekezaji amewekeza asilimia 7.4 kwa walengwa kwenye jumla ya pesa yote ambayo anakuja kuwekeza maana jumla ni billion 426.6 angalieni wenyewe ni billion 31.6. Hawa jamaa wamebenefit sana maana faida watakayoipata kwa huu mradi ni kubwa ndio maana nimeangalia website yao wana offer 22% kama faida kwa mwaka kwa watu watakao invest kwenye kampuni ya hawa jamaa ni ma middle man au kitaalamu ni intermediary. Kweli watanzania bado tumelala ningependa kujua kama huu mradi ni mmoja ya miradi ya serikali iliyo kwenye PPP na kama ni hupo huko naomba serikali ijaribu kuwaelimisha Watanzania juu ya PPP ili wazawa waweze kufaidika zaidi.
ReplyDeleteMdau UK
badala ya kushughulika na ulinzi wako kwenye kukimbizana na wawekezaji.
ReplyDeletePamoja na maelezo marefu mimi nakataa huu uwekezaji. Kwani serikali inashindwa vipi kujenga kituo cha kisasa cha Polisi? Kodi zetu zinakwenda wapi? Hao wawekezaji ndio watakaokuja kuitia mfukoni serikali kwa kupistisha mali zao bila ushuru wala kodi kisa wameisaidia serikali kijengea miundombinu. Maajabu haya yanatokea Tanzania tu, kila kukicha wawekezaji wawekezaji wawekezaji.....
ReplyDeleteTanzania sasa hivi kuna sheria ya PPP (PPP Act 2010). Kwa bahati mbaya sidhani kuwa sheria hii imefuatwa hivyo kwa maana nyingine WIZARA IMEVUNJA SHERIA.
ReplyDeleteJamani tunaelekea wapi sasa?
ReplyDeleteHivi Mamlaka kama Polisi au Wizara ya Mambo ya Ndani na masuala ya uwekezaji wapi na wapi?
Hivi kweli ni busara kuiruhusu Wizara na Idara ya Polisi kuingia Mikataba ya Kibiashara na uwekezaji badala ya ''kusimamia jukumu lao la Kiapo'' la ''Usalama wa Raia na mali zao''?