Fainali ya tuzo za Mwanasoka Bora wa mwaka zinazotolewa na Kampuni ya Wazalendo Bright Media zinatarajiwa kufanyika Desemba 30 mwaka huu jijini Dar es Salaam katika sehemu (venue) ambayo itatangazwa hapo baadaye.

Mchakato wake ulianza tangu Agosti mosi mwaka huu kwa wanamichezo kupigiwa kura na mashabiki kupitia mitandao mbalimbali ikiwemo ile ya kijamii (face book, Twitter na Blogs) na wengine kwa njia ya simu za mikononi kwa kupitia namba maalum.

Kwa sasa kamati ipo kwenye mchakato ya kuchuja majina ambayo yamependekezwa na mashabiki wa soka kupitia kura zao ambapo zaidi ya wachezaji 93 wanaocheza Ligi Kuu Tanzania Bara majina yao yameweza kuonekana ambapo kati ya majina hayo yataopunguzwa na kufikia 30.

Aidha kabla ya kufanyika kwa fainali hiyo wale wachezaji ambao wataingia kwenye fainali watapatiwa semina ya uwezekezaji na ujasiriamali ili kujiandaa na maisha ya baadaye baada ya kustaafu.

Sababu za kufanya semina hii ni kuhakikisha kuwa wachezaji wetu wanapata elimu ya uwezekaji na ujasiriamali ili kuwekeza kwenye sekta mbalimbali kwa ajili ya siku zijazo hasa ikizingatiwa kwamba wachezaji wengi wa Tanzania bado ni masikini.

Kwenye semina hiyo watakuwepo wataalam waliobobea kwenye mambo ya uchumi na fedha ambao watatoa elimu ya uwekezaji, kwa kufanya hivi itawapa nafasi wachezaji hawa kuelewa na kutambua umuhimu wa uwekezaji.

Semina hiyo inatarajiwa kufanyika Desemba 19 na 20 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam. Pamoja semina ambayo itakwenda sambamba na utoaji wa elimu ya afya kwa washiriki wa semina hiyo ambao watakuwa wachezaji pekee.

Imetolewa na

Ahadi Kakore- Mratibu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...