Habari zako kaka Michuzi,
Naamini unaendelea vizuri na kazi zako za kila siku,kaka mimi kama mdau wako namba moja na mpenda maslahi ya watanzania nina jambo linalonitatiza, Mh Rais aliwahi kulitangazia taifa na kueleza taifa kuwa moja ya jambo linalosumbua nchi hii kwa sasa ni usafirishaji wa binadamu,haswa kwa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambayo inasifika sana kwa kuwa na vinara wakubwa wa biashara hiyo.
Je kwanini serikali haijatupa taarifa kama vinara hao wamekwisha kamatwa na je ni kweli wamekamatwa au ni mambo ya fedha na ubabe ambao kwasasa ndo mpango mzima hapa nchini.
Mikoa kama Arusha na Kilimanjaro una vinara wa usafirishaji wa binadamu na pia hadi sasa biashara hiyo inazidi kuwa dili,je usalama wa taifa na jeshi la polisi liko wapi? je uhamiaji umeshindwa kazi zake au ni mpaka al shabab waletwe ndo mtajua adhari za watu hawa? naiomba serikali iwe makini na wakali ili kukomesha biashara hii haramu inayowapa watu utajiri usio na kifani na usio na kodi.
Mdau A Town


Kwanza jiulize kwa nini dawa za kulevya ameshindwa na kwanini biashara ya binadamu inazidi kushamiri!
ReplyDeleteWadau wake ni hao hao wa dawa za kulevya na ni watu 'WANENE' kweli kweli!
Usafirishaji wa binadamu wa kimataifa au wa ndani kwani??fafanua zaidi pliiz.Hata hivyo nakuunga mkono,na mimi napiga vita usafirishaji wa binadamu wa aina yoyote ile.
ReplyDeleteDavid V