Bw Harusi Yusuph Mazimu (Masanja) akiingia kwenye gari tayari kuelekea nyumbani kwa bibi harusi eneo la Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.Nyuma ni mpambe wa Bw Harusi Ustadh Hussein Chifupa.
Kinamama eneo la tukio.Mama mlezi wa Bw Harusi ,Mwalimu Eustela Massatu (Mwenye ushungi 
mweupe)akifuatilia utaratibu wa ndoa ulivyokuwa ukiendelea nyumbani

kwa bibi harusi.
 Sheikh mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Ramadhan Rashid (kulia )akifungisha ndoa Bw Yusuph Mazimu,shughuli  ilifanyika nyumbani kwa bibi harusi Shani Mwakisombole.kulia mwa Bwana Harusi ni Ustaadh Chifupa.
 Mwenyekiti wa BAKWATA Moshi manispaa ,Ustaadh Hussein Chifupa akitoa neno baada ya zoezi la ndoa kukamilika.
 Bwana Harusi katika pozi na wapambe pembeni.
 Wazazi wa Bwana Harusi na Bibi harusi wakifurahia jambo wakati wa ndoa ya watoto wao.kushoto ni Mzee Mazimu,mzazi wa Yusuph Mazimu na kulia kwake ni mzazi wa Bibi Harusi Shanny Mwakisombole,mzee Mwakisombole.
 Bw Harusi Mazimu akifanya dua kabla ya kumfichua Bibi Harusi wake.

Mratibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro (MECKI) Bw,Yusuph Mazimu akiwa katika tabasamu na Bibi Harusi wake Shanny Mwakisombole mara baada ya ndoa yao iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita huko Ally Hassan Mwinyi mkoani Tabora.Bw Mazimu ni mtangazaji wa kituo cha radio cha Moshi fm na Bibi harusi pia ni mtangazaji wa kituo kipya cha radio cha Kibo fm vyote vya mkoani ilimanjaro.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Moshi aliyekuwa mkoani Tabora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera Wanahabari kwa kuanza maisha mapya !

    Mwenyezi Mungu Mkuu na mwingi wa Rehema awaongozee ktk maisha haya mapya.

    Ameeeeeen!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...