Askofu Stephen
Mwakasyuka (1933-2008)
Leo
tarehe 15/11/2012 imetimu miaka minne tangu tulipoondokewa na Baba yetu mpendwa
Askofu Stepen Mwakasyuka. Wakati anaondoka tuliumia mno na wengine kujiona kuwa
na hatia ya kushindwa kufanya kila lililowezekana kuokoa maisha yake.
Tukiwa
bado katika kipindi cha uchungu mkubwa, wakaondoka waliokuwa wakitufariji
wakiwemo akina John Samwel Mwakasungura, Tulinagwe Mbangula, Jimmy David
Ngonya, Kyomba Mwaipopo, na hivi karibuni Jimmy Mwabwagilo, Ashery Mwasandube,
Amon Mwakatobe na Spendi Mwalisatile. Katika hili tumejifunza na kuamini kuwa
ni kweli hapa duniani sote tu wapitaji.
Sisi
tuliobaki katika Familia akina Ezeline, Phoebe, Florence, Jossey, Tungibwaga,
Mponjoli, Atuganile, Frida, Salome, Gwakisa, Christian na Lazaro, tunazidi
kuliwazwa na kufarijiwa na Hazina tuliyonayo ya Ndugu, Jamaa, Marafiki na
Wapendwa waliopo, tukiamini kwamba iko siku sote tutaja onana Paradiso.
Wafilipi
4:6
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...