Mhe. Tuvako Manongi, Balozi wa Kudumu wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akizungumza wakati Baraza Kuu la 67 la Umoja wa Mataifa lilipokutana mwishoni mwa wiki kujadili taarifa ya mwaka ya kazi za Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, na pia kujadili kuhusu ajenda ya kulifanyika mageuzi ya kimfumo ya Baraza hilo kwa kuongeza nafasi za uwakilishi wa kudumu na nafasi zisizo za kudumu. Majadiliano ya kulifanyika mageuzi Baraza hilo yameshadumu kwa zaidi ya miaka 20 sasa na mpaka sasa hakuna dalili zinazoonyesha kwamba mabadiliko yanaweza kutokea mapema iwezekanavyo. Afrika inadai viti viwili vya kudumu vikiwa na haki ya kupiga kura ya vito na pia inataka viti vitano visivyo vya kudumu kwa mujibu wa Makubaliano ya Ezulwini
Home
Unlabelled
KURA YA VETO, MASLAHI BINAFSI NA MISIMAMO YA MAKUNDI VINAPOKWAMISHA KULETA MABADILIKO YA HARAKA KATIKA BARAZA KUU LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ReplyDeleteUkoloni mamboleo at its peak.
Maslahi (Nishati na Madini) na ubabe (Kutawala Dunia) ndiyo vinapelekea Afrika na wenzetu wengine kubinywa.
Watetezi wetu hapo ni warusi na wachina. Wao hawana ndoto za kutawala Dunia.
We Anonymous wa Sat Nov 17, 12:20:00 PM 2012;
ReplyDeleteUnasema nini? Warusi na Wachina hawana ndoto za kututawala?! Huoni wamejaa kibao bongo na misaada yao? Na wachina ndio kabisa wanakimbiza Africa. Yaani hapo hamna kuchagua wote ni mashetani, chaguo lako tu, wote wabaya.