Watanzania wajumuika kwa wingi katika mkutano wa Worldmission Sunday uliofanyika jumapili ya tarehe 28.10.12. watanzania hao ambao walitoka pande mbali mbali za ujerumani, walihudhuria mkutano huo ambao ulianza saa nne asubuhi mpaka saa 6 za mchana. 
Baada ya chakula cha mchana mkutano huo uliendelea hadi saa 12 za jio,i. Dr, Isak Majura alitambulisha Taifa la Tanzania kwa kuonyesha Presentation ambayo ilitayarishwa na Jumuiya ya Watanzania Ujerumani (UTU) Vile vile Katibu wa U T U alionyesha Presentation ya mradi wa shule ya msingi ya iliyopo maeneo ya Kigamboni Dar Es Salaam. ambapo wafadhili kadhaa walionyesha kushawishika sana na kutaka kujua ni jinsi gani wanaweza kuifikia shule hiyo ili kuangalia uwezekano wa kuchangia chochote katika maendeleo ya shule hiyo. Mara baada ya kukamilika kwa presentation hizo Mgeni Rasmi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini ujerumani Bw. Ali Siwa allitoa salam Rasmi kutoka Ubalozi wa Tanzania na kuwashukuru watayarishaji wa Mkutano huo kwa upendo na mualiko kwa Umoja wa Watanzania Ujerumani. Wakati huo huo Bi Tabia Mwanjelwa, (Muimbaji wa Maquiz wa Zamani) aliburudisha kwa kuimba na kupiga gitaa, ambapo aliwaacha hoi wafadhili waliohudhuria katika mkutano huo, Bi Tabia Mwanjelwa alisema sauti yake na utaalamu wake wa kupiga Gitaa ndio mchango wake kwa Watanzania. Watayarishaji wa Mkutano huo wamefurahishwa na wameridhika sana na mahudhurio ya Watanzania, pamoja na presentation zote mbili, na kuahidi kuwa Umoja wa watanzania Ujerumani watapata mialiko mara kwa mara kunapotokea hafla za aina hii. Umoja ni Nguvu ! kamati.utu@googlemail.com
Ni wakati wa msosi
Wadau kibao walikuwapo



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. hivi vazi la kimasai ndio vazi la kitaifa.....au ni vipi? maana naona shughuli watu hupenda kutinga hata katika shughuli za ki-inchi. naomba nijuzwe hapa.

    ReplyDelete
  2. Maskini Mzee Matonya (Mungu amrehemu) alikuwa anaonewa bure wakati wengine tunajisifia umatonya hadi Ujerumani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...