WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MOROGORO NA TASNIA NZIMA YA HABARI NCHINI WAMEPATWA NA MSIBA MKUBWA KUFUATIA KIFO CHA GWIJI WA HABARI NCHINI, MPIGANAJI AIDAN LIBENANGA, ALIYEFARIKI GHAFLA SAA 12 : 15 ASUBUHI YA NOVEMBA 18, MWAKA HUU.
KWA MUJIBU WA NDUGU NA WATOTO WA MAREHEMU, MAZISHI YANATARAJIWA KUFANYIKA NOVEMBA 20, MWAKA HUU( JUMANNE ) MJINI MOROGORO.
BAADHI NI PICHA ZA NDUGU NA MAJIRANI HUSUSANI WAANDISHI WA MOROGORO WAKIWA NYUMBANI KWA MAREHEMU MTAA WA SABASABA.
MAREHEMU ALIKUWA MMOJA WA WAANDISHI WA HABARI WAKONGWE ALIYEWAHI KULITUMIKIA SHIRIKA LA HABARI TANZANIA ( SHIHATA) ENZI HIZO .
Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu 'Libes'
Picha na maelezo na John Nditi.
Hayati Aidan Libenanga
Akina mama wakimfariji mtoto wakike wa Marehemu Aidan Libenanga
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa nyumbani kwa marehemu Aidan Libenanga , eneo la Sabasaba, Mjini Morogoro, akiwasiliana na jamaa zao na kumsikiliza mwanae Rama.
Mtoto wa kwanza wa kiume wa Hassan Libenanga ( kulia) akifarijiwa na kijana mkazi wa Sabasaba
Ramadhan Libenanga (kushoto) mtoto wa marehemu akizungumza na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mstahiki Amiri Nondo, nyumbani kwa marehemu
poleni sana kwa msiba wanafamilia mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu.najua mko ktk kipindi kigumu ila mungu atawawezesha kuwa na subira.inshallah.mzee wetu alikua kiungo mji kasoro ila mola ndiye ajuae.inna lillahi wa inna lillahi rajiuni.
ReplyDeletemayor M.
Poleni sana kina Kuti. Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.
ReplyDeletePoleni sana akina Kuti na Bossnoja
ReplyDeleteRambirambi kwa famili.Poleni.
ReplyDeleteRest in peace kaka Libenanga.
ReplyDelete