Kutokana na maombi ya wadau wengi sana Ankal ameamriwa aweke ngoma moja aipendayo kila siku ili waburudike naye. Basi leo Jumatatu anakuja na ngoma ya Ollie & Jerry ya There's No Stoppin' Us ambayo enzi zao walikuwa wanaimba 'Maiko jakson njooo... sitaaaki. Kama hutaki nendaaaa...' Hii ngoma ilitumika sana kwenye mashindano ya disco ya Break Dance enzi za kina Black Moses,  Ommy Sydney, Athumani Digadiga, Abdul Shalamar na wengineo - kwa mnaokumbuka leteni data zaidi....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Dancers wa zama zile msimsahau RAY ABDU, Mkali wa kucheza mwenye vituko na mwenye majina mengi.

    Alikuwa ananyoa nywele mitindo ya ajabu ajabu na kuvaa kiajabu ajabu huku akicheza Muziki kiajabu ajabu.

    Nilishuhudia siku moja akitaja majina zaidi ya 32

    -RAY MANGA,
    -PAKA SHUME
    -(,,,mwaga haja ndogo,,,)
    -GOLOGOTA
    -AWOLOWO
    -DZANIMBI
    -ADEDEJI

    ..........na mwengine kibao hadi 32

    La ajabu aliambiwa ayarudie kuyataja hakukosea hata moja!

    ReplyDelete
  2. OLD TIME DANCERS LIST:

    .Black Mosses
    .Ommy Sydney
    .Athumani Digadiga

    Wengine ni

    .TASS Chiume
    .Paylonga (DJ & Dancer)
    .Ray Abdu-Adedeji

    ReplyDelete
  3. Acha mambo wewe Pai hakuwa dancer alikuwa brother man tu, ma dancer walikuwa kina Tasi,Digadiga, Mzee Bachu, Ommy Sidney, Abdul Shalamar, Raju, Rumi na Khairoon (baba na mama wa bob junior) na kina black moses. Kama ulikuwa hujafika mjini bado unaweza kuuliza tu au vipi...du kinaa

    ReplyDelete
  4. Mdau wa 3 anonymous wa Mon Nov 19, 08:38:00 PM 2012

    Kinachochangiwa hapa sio nani ni zaidi, tunachangia kumbukumbu tu!

    Kama unaelewa mengi toa mchango wako kistaarabu zaidi ili watu wafaidike...ni hilo tu.

    ReplyDelete
  5. Mtoa maoni wa (3) anony Mon Nov 19, 08:38:00 PM 2012

    Anawakilisha mamia kwa mamilioni ya Watanzania ambapo mahala pa majadiliano analeta kashfa kejeli na dharau kwa wengine.

    Je kwa mwendo huu tutajenga au tutamoboa?

    Je, kama Muungwana Muhiddin Issa Michuzi(Mhe.Balozi),Ankali Mwanalibeneke angekuwa na tabia mbovu kama wewe tungetoka kweli?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...