Akizungumza
na wandishi wa habari Katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo),jijini
Dar es Salaam leo, mama wa mtoto huyo, Veronika Laurent ambaye ni Mkazi
wa Bunju, alisema mtoto huyo alizaliwa huku akiwa na sehemu ya kutolea
haja kubwa lakini cha kushangaza, haja kubwa ilikuwa ikitokea mdomoni.
Alisema
msaada wa fedha hizo utasaidia katika kumfanyia operesheni mtoto huyo
ambaye kwa sasa anaishi akiwa katika mateso makubwa.
Veronika
alisema hivi sasa yeye pamoja na mwanaye huyo wanaishi maisha ya
kubahatisha baada ya baba wa mtotohuyo kuitelekeza familia hiyo kutokana
na hali ya ugonjwa wa mtoto huyo.
“Mimi
ni nachoomba ni msaada wa fedha ili niweze kumpeleka kwenye matibabu
kwani sina msaada wowote,ukichukulia wazazi wangu kufariki na hivi sasa
naishi kwenye nyumba ya mwenyekiti wa Mtaa wa Bunju wilayani Kinondoni
jijini baada ya kushindwa kupangisha chumba kwani sina kazi
yeyote”alisema.
Aidha,
alisema hadi utumbo wa mtoto huyo kutoka nje, ni baada ya kufanyiwa
operesheni katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo hata
alipompeleka tena kwa ajili ya matibabu alikosa ushirikiano kutoka kwa
madaktari na wahudumu wengine.
Alisema
kwa yeyote ambaye yuko tayari kumsaidia anaweza wasiliana naye kwa
kupiga simu namba o715 83 77 00, na namba ya mwenyekiti huyo wa mtaa
0656780236.
Veronika
ni mzaliwa wa Mkoa wa Kilimanjaro eneo la Kijiji cha Uru,Moshi ambye
alimzaa mtoto huyo na mwanamme aliyemtaja kwa jina la Abdalah Said,
kabilake makonde mfanyabiashara wa viatu Ubungo.
ALLAH AKBAR... UNCLE KAMA UNAWEZA TUTAFTIE M-PESA YA HUYO DADA TUMSAIDIE CHOCHOTE. SHUKRAN KWA TAARIFA.
ReplyDeleteJamani kuna madakari wengi tangia mkunga, madaktari wa muhimbili ambao wamemuona mtoto huyo na matatizo yake lakini hakuna hata mmoja aliyeguswa na kujitolea kumsaidia mtoto huyu mapema hadi amekuwa mkubwa. Pia hospitali kubwa ya muhimbili imekataa kumsaidia mtoto huyu, jamani tunaenda wapi? Mama kapige kambi Getini wizara ya Afya. alexbura dar
ReplyDeleteAnony 06.49.00. Asante kwa maoni yako. Hata akienda hapo Wizara ya Afya unadhani watafanya kitu? Sanasana watampeleka Muhimbili halafu ataanza kupigwa tarehe za njoo baada ya wiki, kisha mwezi haya mwaka mwingine tena. Hii Wizara ya Afya inatengewa pesa nyingi sana hata sijui VIPAUMBELE VYAO NI VIPI? Sijui kama huwa wana issue za haraka kweli!!! Niliwahi kuona mtoto wa namna hii na wazazi wake walikuwa hawana uwezo kutokea Zanzibar (akigharamiwa na Serikari ya Mapinduzi) alikuja hosp. binafsi hapa Dar kwa ajili ya operesheni hiyo na ilifanikiwa. Si kwamba Muhimbili hawawezi lah! Walipeni vizuri hao jamani na vifaa wanaweza, SIO KILA KITU INDIA!!! Mbona kwenye Hospitali binafsi wanazifanya???
ReplyDeletePole sana mama, natumai utapata msaada lakini kwa ushauri wa haraka haraka nimepata kuona Mcungaji Kakobe akidai kuponyesha, je ummemjaribu? Hata mchungaji Lusekelo pia anaponyesha, natumai watasikia kilio chako, hata kama wao hawaingii kwenye mablog nina uhakika kuna waumini wao watafikisha kilio chako, pole sana.
ReplyDeleteBaba yake kama yupo kwanini asimshughulikie au mmetengana?Jamani mtoto anateseka sana huyo.Nitampigia huyu mama anieleze vizuri zaidi.
ReplyDeleteSiyo kwamba wamekataa kumsaidia, pengine HAWAWEZI KUMSAIDIA, in that case wampeleke India kama wanavyojipeleka wao na familia zao.
ReplyDeleteEEEE bwana eehhhh!Inshallahh ,haujazaliwa haujafa na haujafa haujazaliwa.Yaani bongo madaktari kibao ,hospital kibao na matajiri kibao ,jamani huyu mtoto kwa kweli watu kibao ni matajiri wanashindwa kumsaidia?Basi serkali iingilie kati ,fedha kibao za walipa kodi na misaada inayotolewa kwa ajili ya watoto walioko ktk mazingira magumu.Gazeti la mwananchi limeandika hivi karibuni Tanzania ni nchi ya kwanza duniani inayoongoza kwa kupatiwa misaada na mataifa matajiri,je misaada hiyo inaishia wapi?Walengwa wa misaada hiyo ni kama huyu mtoto au?UNICEF ,etc mko wapi?Matajiri mlioficha fedha uswis je mnamuona huyu mtoto?Bro michuzi fanya mpango mtoto huyu aonyeshwe hata kwenye TV live ili watu wenye uwezo wamchangie.Yaani akina Lowasa wakiumwa kichwa tuu wanaruka ughaibuni kutibiwa na wengineo kibao,je vipi huyu dogo?Madaktari Muhimbili etc muwe na utu sio kuangalia sana fedha ,huyu dogo tatizo alilonalo mnaweza kumtibu hapo bongo na mimi naongea kama mtu mwenye ujuzi kidogo na ninajua anaweza kuwekewa anuspreta na akatibiwa ,ni simple mtu kama ni mtaalamu na wataalamu tunao hapo bongo.Dogo na mama yako nawaombea kila la heri ,hatimaye msaada utaupata.Mdau
ReplyDeleteeee mungu...
ReplyDeleteDont make excuse ya nani asaidie. Mimi na wewe tusaidie acheni maelezo ya kusukumia na kulaumu wengine. Upendo wako ni muhimu kuliko madaktari, wizara, matajiri, mawaziri nk. Do something now na stop yawning.
ReplyDeleteBinasfi nitasaidia. Nawewe saidia. Stop pointing fingers
anonymous 05:43:00 uko sahihi kabisa. Tuchange ili mtoto apone. tuache kulalmika kuwa hao wengine wanapesa. watu wa kipato cha chini/kati 300 wakichanga kila mmoja 20,000 tunaweza kumponya mtoto huyu na tunaweza. Hima tumchangie mtoto huyu. Mimi kesho natoa mchango wangu. Mungu msaidie mtoto huyu apate matibabu. Tungependa tuje tupate feedback ya afya yake.
ReplyDelete