Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini TACAIDS, Dk Fatma Mrisho akizungumza mbele ya ujumbe wa watu kutoka nchi mbalimbali waliofika kwenye ofisi za shirika la vijana la Tayoa kumpongeza mkurugenzi wa shirika hilo, Peter Masika kwa kushinda tuzo maalum ya kupambana na Ukimwi. , Dk. Mrisho aliongoza ujumbe wa watu mbalimbali kwenda kulipongeza shirika hilo kwa kupata tuzo ya kupambana na Ukimwi.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la vijana Tayoa Peter Masika, akimwelekeza Mwenyekiti wa Tume ya KUdhibiti Ukimwi TACAIDS, Dk Fatma Mrisho namna ambavyo simu za bure za kuelimisha wananchi kuhusu UKimwi zinavyofanyakazi, Dk. Mrisho aliongoza ujumbe wa watu wa mataifa mbalimbali kwenda kulipongeza shirika hilo kwa kupata tuzo ya kupambana na Ukimwi.
Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini TACAIDS, Dk Fatma Mrisho akiuliza jambo kupata ufafanuzi kuhusu mtambo wa kupokea ujumbe (sms) wa shirika la vijana Tayoa wakati yeye na ujumbe wa watu kutoka mataifa mbalimbali walipokwenda kulipongeza shirika hilo kwa kupata tuzo ya kupambana na Ukimwi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...